Augustine Okrah akifunga mbele ya mlinda mlango wa Yanga Augustine Okrah
Ligi Kuu

Jinsi wageni wanavyowakimbiza wazawa Ligi Kuu.

Sambaza....

Ligi Kuu ya NBC imefikisha michezo 25 mpaka sasa huku ikiwa imesalia michezo michache pekee ligi hiyo namba tano kwa ubora Afrika imalizike.

Mpaka sasa Yanga ndie kinara akiwa kileleni na alama zake 65 akifuatiwa na hasimu wake Simba mwenye alama 57 wakiwa mbele ya Singida Big Stars [48] na Azam Fc [47] katika nafasi ya tatu na nne.

 

Achana na ubabe huo wa vigogo wa nchi katika msimamo wa Ligi, upande wa pili kwenye takwimu za mchezaji mmoja mmoja wachezaji wakigeni wameonekana kufanya vizuri na kuwakimbiza wazawa.

Katika chati ya ufungaji mabao, wachezaji waliohusika katika mabao mengi na walinda mlango waliotoka uwanjani wakiwa hawajafungwa imeonekana kutawaliwa na wachezaji wa kigeni.

Fiston Mayele akishangilia bao lake dhidi ya Singida Big Stars

Katika ufungaji kinara ni mshambuliaji wa Yanga raia wa Congo DR Fiston Mayele mwenye mabao 15 akifwatiwa pia na wageni kutoka Simba Saidoo Ntibazonkiza [Burundi] na Moses Phiri [Zambia] wenye mabao kumi kila mmoja. Baada ya hapo ndio anakuja wazawa John Bocco kutoka Simba na Sixtus Sabilo wa Mbeya City wakiwa na mabao 9 wakifungana na Mbrazil Bruno Gomes wa Singida Big Stars.

Katika upande wa wachezaji wanaohusika kwa mabao mengi kwa maana ya kufunga magoli na pasi za mabao bado wanasimama katika chati ni Saido Ntibazonkiza aliyehusika katika mabao 19 akifuatiwa na Clatous Chama na Fiston Mayele waliohusika katika mabao 17. Baada yao ndio anakuja mzawa Sixtus Sabilo wa Mbeya City aliyehusika katika mabao 16.

Bruno Gomes.

Kwa upande wa makipa mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya Mali na Yanga Djigui Diara anawakimbina makipa wazawa kwa ana “clean sheet” nyingi 14 akifwatiwa na Aishi Manula wa Simba mwenye “clean sheet” 12 na wamwisho kwenye tatu bora ni kipa wa Commoro na Azam Fc Ally Ahamada mwenye clean sheet nane.

Sambaza....