Meddie KagereMeddie Kagere (Simba Sc)
Ligi Kuu

Kagere akabidhiwa kiatu cha kandanda

Sambaza....

Mtandao wa Kandanda leo umemkabidhi zawadi zake mshambuliaji wa klabu ya Simba, Meddie Kagere, baada ya kuifungia klabu hiyo mabao sita (6) katika ligi ya Vodacom Tanzania bara mwezi Agosti-Septemba.

Kandanda inautaratibu wa kumzawadia Galacha wa mabao wa kandanda, ambayo kwa sasa inadhaminiwa na Mgahawa Café & Restaurant na FYN By Falsafa. Utaratibu huu ulianza msimu uliopita na sasa unaendelea ukiwa umeboreshwa zaidi.

Kagere alikabidhiwa kiatu cha mpira wa miguu, body splay ya fyn, pia atapata chakula cha usiku katika mgahawa wa Mgahawa Café ikiwa ni sehemu ya kumpongeza kwa kuwa galacha wa mabao wa mwezi agosti-septemba Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Kwa upande wake Kagere ameushukuru mtandao wa kandanda kwa kuendelea kutambua juhudi zake katika kupachika mabao. Jumapili hii atakuwa tena uwanjani tena katika kuisaidia klabu yake kuendelea kuongoza ligi, mtandao wa Kandanda unamtakia kila la kheri.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.