Shomary Kapombe
Mabingwa Afrika

Kapombe: Mechi na Raja Casablanca ni sehemu ya maandalizi

Sambaza....

Mlinzi wa pembeni wa Simba Sc Shomary Kapombe pamoja na wachezaji wenzake ambao hawajaitwa katika timu zao za Taifa wameendelea kujifua kuelekea mchezo wa mwisho wa kundi C wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.

Kuelekea mchezo huo ambao ni wakukamilisha tuu ratiba kwani timu zote mbili tayari zimefuzu kwenda hatua ya robo fainali Shomary Kapombe amesema wao kama wachezaji watautumia kama sehemu ya maandalizi kuelekea michezo ya robo fainali.

“Mchezo utakuwa mgumu, Raja ni timu kubwa Afrika na tunaenda kwao. Tayari tumefanikiwa kutinga robo fainali hivyo tutautumia mchezo dhidi ya Raja kama sehemu ya maandalizi sababu ni mechi ya mwisho ya kundi,” alisema Shomary Kapombe.

Mlinzi huyo wa pembeni wa zamani wa Azam Fc ameyasema hayo akizungumza na tovuti ya klabu yake ya Simba. Kwasasa Shomary hajaitwa kikosini Stars kiasi cha kupelekea wadau wa soka kutoa maoni tofauti na kuwa gumzo baada ya uteuzi huo wa kocha mpya wa Stars Adel Ameorouche.

 

Sambaza....