Sambaza....

Ikiwa ni hatua ya 16 bora ya mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya, tukishuhudia  vilabu vya Ajax, Atletico, Barcelona, Bayern Munich, Dortimond, Juventus, Liverpool na Lyon zikifuzu kwa kuongoza katika makundi yao  huku Man City, Man U, PSG, Porto, Real Madrid, Roma, Schalke na Tottenham nazo zikiungana katika hatua hii zikiwa katika nafasi ya pili.

Droo inayotarajiwa kuchezeshwa hivi karibu na wote tunatarajia vilabu vilivyofuzu katika nafasi ya kwanza vikikutana na vilabu vilivyofuzu katika nafasi ya pili huku timu kutoka taifa moja kutokutana, na hii ni kwa mujibu wa sheria za shirikisho barani ulaya (UEFA).

Hadi mashindano haya yanaingia katika hatua ya mtoano, inamuonesha Robert Lewandowski akiwa kinara wa kupachika mabao, tayari ameshafanya hivyo mara 8 huku magoli mawili kati ya hayo akifunga kwa mikwaju ya penati. Lionel Messi ana magoli 6, Paul Dybala wa Juve ana goli 5 akiwa sawa na Edin Dzeko wa AS Roma na Andrej Kramanik wa Hoffenheim.

Kuna mtu mmoja anakosekana kwenye hiyo orodha ambaye ndiye “mchawi” wa  kufunga katika michuano hii naye si mwingine bali ni Christiano Ronaldo.

Namuita “mchawi” nikiwa nina maana nzuri kwakuwa yeye ndiye mwenye rekodi nyingi na michuano hii. Ronaldo ndiye mchezaji pekee ambaye amechukua kiatu cha ufungaji bora  katika michuano hii mara 4 mfululizo.

Msimu wa 2007/08 ndio msimu wake wa kwanza kuwa mfungaji bora wa michuano hii akiwa na Man U na kufunga magoli 8 pekee, baada ya hapo Lionel Messi alifululiza misimu mitatu, yaani kuanzia msimu wa 2008/09 hadi 2011/12.

Msimu wa 2012/13 akiwa real Madrid, Ronaldo alichukuakiatu akiwa na magoli 12, msimu 2013/14 alichukua tena akiwa na magoli 17 nakuweka rekodi mpya ya kufunga magoli mengi zaidi kuwahi kutokea kwa msimu,msimu wa 2014/15 walikuwa na magoli sawa wachezaji watatu, Ronaldo, Neymar naMessi wa Barcelona wote wakiwa na magoli 10, Msimu wa 2015/16 Ronaldo alichukuatena kiatu hicho akiwa na magoli 16 akikaribia kuifikia rekodi aliyoiwekamwenyewe.

Katika michuano hii, Ronaldo ndiye mchezaji pekee mwenye magoli mengi zaidi, anayo 120, anashikiria rekodi ya kuwa mfungaji bora wa msimu, magoli 17 msimu wa 2013/14, na  ndiye mchezaji pekee aliyeshinda fainali 5 za michuano hii,  maana yake kila akiingia fainali lazima abebe ndoo.

Messi

Ndiye mchezaji pekee aliyefunga goli katika fainali tatu alizocheza, ndiye mchezaji pekee aliyefunga katika kila mchezo katika mechi 6 za makundi ya michuano hii, ndiye mchezaji pekee kufunga magoli 11 mfululizo, ndiye nguli pekee aliyeifunga timu moja magoli mengi zaidi, magoli 10 akiifunga timu yake ya sasa, Juventus.

Katika msimu huu, Ronaldo amefunga goli 1 pekee na kutoa pasi za mwisho 3 huku kukiwa na tofauti ya magoli 7 na Lewandowski anayeongoza kwa magoli 8.

Lewandoski

Kwa Yule mwenye kumbukumbu nzuri, katika msimu uliopitaakiwa na Real Madrid alianza micghuano hii pamoja na ligi  kwa kusuasua, na wengi wakidhani huenda ameshachokayaani “ amefulia” kumbe ilikuwa ni tofauti, Ronaldo alianza kufunga mfululizona hadi mwisho wa mashindano hayo alikuwa na magoli 16 akiwazidi Sadio Mane, Mo Salah  na Roberto Firmino wa Liverpool wote wakiwa na magoli 10.

Kwa rekodi zake na uzoefu aliokuwa nao alitazamapo goli, bila shaka sio mtu wa kubeba hata kidogo ,anaweza akafanya vizuri zaidi hadi watu wakashangaa. Hata hivyo anayeongoza  kwa ufungaji , Lewandowski na timu yake ya Bayern Munich bado hawako vizuri na hii ina maana kuwa mbio za Mpolandi huyo huenda zikaishia karibu.

RONALDO  mwenyewe anasemaje?

Baada ya jana kumaliza mchezo dhidi ya Young Boys katika kundi H, licha ya kupoteza kwa 2-1, na Ronaldo kutofunga goli, alionekana kujiamini na kusema kuwa muda wake wa kuibeba Juventus umewadia.

Ronaldo amesema kuwa, hatua inayofuata ni ngumu lakini anaimani, vitu vizuri kutoka kwake na timu kwa ujumla vinakuja. Bila shaka kauli yake hii inaoneha jinsi gani anavyoiwazia tuzo ya mfungaji bora licha ya kuwa nagoli moja pekee.

Ronaldo amewaahidi mashabiki wa Juve na mashabiki wkae duniani kote kuwa atafanya juhudi ili kuifikisha timu yake mbali, hivyo hawatakiwi kuwaza matokea ya mchezo wao wa mwisho dhidi ya Young Boys.

Je unahisi Ronaldo atachukua kiatu msimu huu licha ya kuwa na goli 1?, vipi kuhusu nafasi ya Lewandowski na Messi? Tutaona.

Sambaza....