Uhamisho

Kichuya kumkimbia Morrison Simba

Sambaza....

Baada ya kukosa namba katika klabu ya Simba tangu arejee kutoka Misri alipobahatika kucheza soka la kulipwa , Shiza Ramadhani Kichuya anaonekana kutaka kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.

Shiza Ramadhani Kichuya alisajiliwa na Simba akitokea kwenye klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. Mipango bado inaendelea ili kiungo huyo hatari anayetumia mguu wa kushoto kurudi katika klabu yake hiyo ya zamani.

Kichuya

Mtibwa Sugar iko katika hatua nzuri ya mazungumzo ya kumsajili kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya ambaye amemaliza mkataba wake wa miezi sita Msimbazi. Tangu arejee Simba akitokea klabu ya Pharco ya nchini Misri, Kichuya amekosa nafasi katika kikosi cha kocha Sven Vandenbroeck.

Shiza Ramadhani Kichuya kwa sasa inaonekana nafasi yake ni finyu kutokana na Simba kumsajili Bernard Morrison kwa ajili ya msimu ujao.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.