Ligi

Kina Ajib wameridhika sana- Kocha wa Simba

Sambaza....

Simba jana imeongeza pengo la alama kati yake na Yanga na kufikia alama 10, ambapo Simba ina alama 34 na Yanga ina alama 24 na hii ni Baada ya Simba kushinda mechi ya Jana magoli 2-0, magoli ya Deo Kanda na Francis Kahata.

Akizungumza Baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Simba amedai kuwa amefurahishwa na urejeo wa John Bocco na Erasto Nyoni katika mechi hiyo.

“Nimefurahia Erasto Nyoni na John Bocco wakimaliza dakika zote tisini katika mchezo wa Leo, nimefurahia kuona Deo Kanda na Francis Kahata wakifunga , lakini sijafurahishwa na jinsi timu inavyocheza”.

“Kuna baadhi ya wachezaji wanaona hii ni timu kubwa, hata kama ni timu kubwa tunatakiwa kupambana ili kupata ushindi , siyo kwamba timu kubwa na ushindi utakuja”. Alimalizia Kocha huyo, Simba kwa sasa inajiandaa na mechi ya tarehe 4 dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa uhuru.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.