Ismail Sawadogo
Uhamisho

Kiongozi Simba: Sawadogo ni Yaya Toure Mtupu.

Sambaza....

Klabu ya Simba imeendeleza pale ilipoishia katika kusafisha timu yao na sasa panga limemuangukia kiungo Ismael Sawadogo ambae hapo jana alipewa mkono wa kwaheri.

Kama ilivyoada neno “Thank you” limeendelea kutamba katika kipindi hiki na afisa habari wa Simba Ahmed Ally anakiri Sawadogo ni mchezaji mzuri tatizo ni muda aliofika Simba huku akimfananisha na kiungo kutoka Ivory Coast Yaya Toure.

Baada ya Simba kutangaza kuachana na Sawadogo rasmi Ahmed Ally alisema “Mashabiki wengi wa Lunyasi wamefurahi kuondoka kwa Ismael Sawadogo” alisema na kuongeza :Kama mchezaji inaumiza kuona watu wanafurahia kuondoka kwako na kwa kiongozi inaumiza kuona uliyemsajili amewapa furaha watu siku ya kuondoka.”

Ismael Sawadogo.

“Sio kama wanamchukia ila hawakupata walichotaka kutoka kwake. Lakini furaha ya Wana Simba sio kuondoka kwa Sawadogo, furaha yao ni kwa sababu wana matumaini atakuja mtu bora zaidi.”

Sawadogo ni mchezaji wa daraja la juu kama angepata muda dunia ingemuona tena Yaya Toure akiwa na jezi nyekundu. Shida iliyopo wana Simba hawana muda wa kumsubiri mtu. Wana Simba wanakimbia hivyo hawapo tayari kuongozana na mtu anaetembea. Na haya ndio maisha ya Kibebari yalivyo,” alimalizia Ahmed

Nae mwanahabari mwandamizi Abdul Mkeyenge ametoa maoni yake baada ya kuachwa kwa Sawadogo huku akionyeshwa kutokishangazwa na maamuzi hayo ya Simba.

“Ismail Sawadogo amepewa “Thank you” Msimbazi. Nadhani haishitui wala haishangazi. Kila mmoja alikuwa anaitabiria na kuisubiri “Thank you” hii. Wasifu wake Sawadogo unatisha na unatamanisha. Alikopita ni mahala pazuri. Ni rahisi kuzivutia timu nyingi kuitaka huduma yake. Kila la kheri Sawadogo,” alisema Mkeyenge.

Sambaza....