Kocha Mkwasa
Ligi Kuu

Kisa cha Molinga na Mkwasa hiki hapa!

Sambaza....

Hali ya kutoelewana kati ya David Molinga na kocha msaidizi wa Yanga , Charles Boniface Mkwasa imekuwa kubwa baada ya David Molinga kufikia hatua ya kuongea na vyombo vya habari na kudai kuwa kocha huyo msaidizi wa Yanga hampendi David Molinga.

David Molinga amedai hayo baada ya Charles Boniface Mkwasa kumwacha David Molinga kwenye kikosi cha Yanga SC kwa madai kuwa Molinga kwa sasa hana “fitness” nzuri na ameongezeka kilo 12 mpaka sasa hivi.

Kitu ambacho David Molinga amekikataa kwa sababu wachezaji wengi hawana “fitness” kwa mujibu wa madai yake kutokana na wachezaji wengi kuwepo Quarantine kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa Corona.

David Molinga “Falcao”

David Molinga pia anadai kuwa yeye hajazidi kilo 12 kama inavyodaiwa na kocha huyo msaidizi wa Yanga , Charles Boniface Mkwasa . David Molinga amedai kuwa yeye kazidi kilo 3 tu na siyo kilo 12 kama inavyodaiwa.

Mgogoro huu kati ya David Molinga na Charles Boniface Mkwasa ulianza kwenye mechi dhidi ya Ndanda FC baada ya Charles Boniface Mkwasa kumtoa kipindi cha kwanza David Molinga . Tangu muda huo David Molinga amekuwa na mtazamo kuwa Charles Boniface Mkwasa hampendi David Molinga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.