Uhamisho

Kiyombo ni mchezaji halali wa MAMELOD SUNDOWNS

Sambaza....

Nyota wa klabu ya Singida United Habibu Kyombo “Griezman” anaeitumikia klabu ya Singida United amezua maswali mengi baada ya kuonekana amefuzu majaribio katika klabu ya Mamelody Sundowns lakini bado akiendelea kuonekana nchini.

Mwaka jana kulikuwa na habari za Habib Kiyombo kwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika kusini. Taarifa za majaribio hayo zilidai kuwa Habib Kiyombo alifanikiwa kufuzu majaribio hayo na akapewa mkataba rasmi na klabu hiyo.

Lakini tatizo kwa watu lilibaki pale walipoendelea kumuona Habib Kiyombo akiwa bado anaitumikia klabu ya Singida United wakati ilidaiwa kuwa amesaini mkataba na Mamelod Sundowns.

Tovuti yako ya Kandanda.co.tz iliamua kumtafuta Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga ili kutupa ukweli wa taarifa hizi.

Festo Sanga amedai kuwa Habib Kiyombo ni mchezaji halali wa Mamelod Sundowns. Kinachomfanya kuendelea awepo Singida United ni makubaliano ya pande zote mbili.

“Singida United tuliwaomba Mamelod Sundowns tumtumie Habib Kiyombo mpaka mwishoni mwa msimu huu ili atusaidie msimu huu kwenye michuano mbalimbali.”

“Tuna lengo la kumaliza katika nafasi za juu kwenye ligi kuu ya Tanzania bara. Pia tunalengo la kuchukua kombe la Fa ili wapate nafasi ya kuiwakilisha Tanzania.

Ndiyo maana tukawaomba Mamelod Sundowns watupe Habib Kiyombo atusaidie kwa msimu huu na msimu ukimalizika ndipo ataenda Afrika Kusini”.

Kwa ufafanuzi huo basi msimu Habibu Kyombo atajiunga na klabu yake mpya ya Mamelody Sundowns mwanzoni mwa msimu wa 2019/2020.

 

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.