Ally Ramadhani "Oviedo" akiwa mazoezini katika uwanja wa Bora Kijitonyama.
Ligi Kuu

KMC yaanza mazoezi!

Sambaza....


Klabu ya soka inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni KMC fc tayari imeitikia kauli ya rais ya kurudisha michezo na tayari wameingia kambini kujiandaa na kumalizia michezo iliyokabi ya Ligi.

Kmc imeanza mazoezi tangu siku ya Jummane tarehe 26 katika uwanja wa Bora Kijitonyama, huku wakiweka kambi yao maeneo ya Makongo Juu karibu na Chuo cha Kikuu cha Ardhi.

Mpaka Ligi inasimama kutokana na ugonjwa wa corona KMC unashika nafasi ya 15 ikiwa na alama 33 huku ikiwa imeshuka dimbani mara 29. Kabla ya Ligi kusimama KMC ilikua katika muendelezo mzuri baada ya kushinda michezo minne mfululizo na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kujitoa katika eneo hatari la kushuka daraja.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.