Ligi Kuu

KMC Yamfukuza Hitimana, Kocha wa Simba Apewa Kazi

Sambaza....

Klabu ya soka ya KMC Fc inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni leo imetangaza kuachana na kocha wake Hitimana Thiery baada ya muenendo mbovu wa timu yao.

Taarifa ya klabu hiyo imetanabaisha kuwa baada ya bodi kukaa na kujadili muenendo wa timu na kutoridhishwa nao sasa wameamua kulivunja benchi lote la ufundi.

 

“Bodi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni [KMC FC] baada ya kukaa kikao leo mapema asubuhi imeamua kuvunja benchi lote la ufundi lililokua likiongozwa na Kocha Hitimana Thiery baada ya kufikia makubaliano kutokana na kutoridhishwa na muenendo wa timu msimu huu,” ilisema taarifa hiyo

Katika hatua nyingine timu hiyo ya Manispaa imeamu kumkabidhi timu hiyo kocha wa zamani na mchezaji wa zamani wa Simba Sc Jamhuri Kihwelo Julio ili aweze kuinusuru timu isishuke daraja.

Jamhuri Kihwelo Julio.

“Uongozi umefikia makubaliano na kocha Jamhuri Kihwelo Julio ambae atachukua timu pamoja na benchi lake la ufundi,” ilimalizia taarifa hiyo

Mpaka sasa KMC inashika nafasi ya 14 ikiwa na alama 26 katika michezo 26 iliyoshuka dimbani na kuwafanya wawe katika nafasi ya kucheza “Playoffs” huku wakiwa na alama sita juu ya mstari wa kushuka daraja. 

 

Sambaza....