Luc Aymael kocha mkuu wa Yanga sc.
Ligi Kuu

Kocha aitaka Yanga kuonyesha ukubwa wake!

Sambaza....

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Luc Aymael ameonyesha kusikitishwa na klabu yake pamoja na wadhamini wa klabu yake kushindwa kumrejeshi nchini kwa wakati. Luc Aymael kwasasa yupo kwao nchini  Ubelgiji baada ya kuondoka nchini kutokana na janga la virusi vya corona.

Luc Aymael ameongea na mtandao wa goal.com na kuonyesha ni jinsi gani hapendezwi na hali ilivyo na kuonyesha waziwazi ni kiasi gani hafurahishwi na hali hiyo.

Luc Aymael “Kama nilivyokuambia, wao [maafisa wa Yanga] wananiambia kuwa hawawezi kunikatia tiketi ya ndege kwenye “system” ikiwa hawawezi kuniwekea “booking” kwenye “system” basi wanapaswa kujaribu kunikatia tiketi yangu mtandaoni, ni rahisi unajua.

Kocha wa Yanga Luc Aymael (kushoto) na kocha wa Simba Sven Van Debroek.

Ni vizuri kusaini mkataba na La Liga lakini ikiwa unataka kuwa klabu kubwa, basi, kwanza, jaribu kumrudisha kocha wako mapema iwezekanavyo ikiwa unamuheshimu kocha wako. Naona wachezaji wa Simba SC wao walirudi kutoka kila mahali,  kocha wa Azam FC pia alifika kutoka Romania, alisafiri kutoka Romania kwenda Frankfurt, kisha kwenda Ethiopia na mwishowe jijini Dar es salaam.”

Baada ya michezo kuruhusiwa nchini tayari makocha na wachezaji mbalimbali wanaotoka nje ya nchi wamerejea nchini tayari kabisa kwa kuanza kutumia klabu zao.

Klabu ya Yanga imepangwa kuanza kufungua dimba na Mwadui fc siku ya Jumamosi tarehe 13 katika uwanja wa Kambarage Shinyanga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.