Said Hamis Ndemla.
Blog

Kocha amkomalia kiungo Simba.

Sambaza kwa marafiki....

Mwalimu wa viungo wa Simba Abel Zrane leo katika mazoezi ya Simba leo Bokko Beach ameonyesha hataki masihara katika ufiti wa wachezaji wake baada ya kukomaa na kiungo matata wa Wekundu wa Msimbazi.

Katika mazoezi hayo baada ya mwalimu mkuu Patrick Auseems kugawa vikosi viwili na kucheza “full game” wachezaji watatu wa Simba walibaki nje wakiwatazama wenzao wakicheza ndani ya uwanja.

Waliokua nje ni pamoja na kipa Ally Salim, Yusuph Mlipili na kiungo Said Ndemla waliokua wamekaa nyuma ya goli. Lakini mwalimu wa viungo wa Simba aliwafuata hukohuko huku akiwa amebeba vifaa vya kujenga mwili.

Katika mazoezi hayo ya viungo mwalimu alionekana kumfwatilia zaidi Said Ndemla huku akikaa nae kwa ukaribu. Ndemla ambae ni kipenzi cha mashabiki wa soka wa Tanzania alionyesha kumudu mazoezi hayo bila shida yoyote.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.