EPL

Kocha mpya wa Man U, Ole Gunnar apangua maswali ya waandishi wa habari.

Sambaza....

Tovuti hii inakuletea mkutano wa kwanza wa kocha wa muda wa Mashetani Wekundi, Manchester United Ole Gunnar na waandishi wa habari uliofanyika jana tarehe 21-12-2018 kufuatia upya wake katika klabu na mechi dhidi ya Cardiff city jumamosi hii.

Mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari ulichukua takribani dakika 10 na sekunde 37. Huku waandishi wakipata nafasi ya kuuliza maswali 13 Na mambo yalikuwa kama hiviii…

Mwandishi: Vipi ulipopata simu kutoka klabuni, ulihisi kabisa simu hiyo ingekutaka wewe kuwa kocha wa Man U?

Ole Gunnar Solskjaer: Hapana ! hapana, sikuhisi hivyo, lakini najihisi furaha kuwa hapa na kuisaidia klabu, naweza sema hivyo.

Mwandishi: Ni kazi gani ndani ya klabu umeambiwa unatakiwa kuifanya?

Ole Gunnar Solskjaer:kuwa na klabu, kufanya mambo yote ya kikocha ndani ya miezi sita na kabla ya timu haijapata kocha wa kudumu.

Mwandishi: Wachezaji wapo katika hali gani, umezunguza nao?

Ole Gunnar Solskjaer:Wanafaraha ! Nimekutana na wachezaji na wengine katika bodi ya timu, unajua wengine nilikuwa nao hapa  lakini wengi ni wapya !

Mwandishi:Je wamekwambia kuhusu suala la kusalia kama kocha mkuu na wa kudumu endapo utafanya vizuri katika kipindi hiki cha miezi sita ?

Ole Gunnar Solskjaer: Unajua ukipata kazi kwenye klabu kama hii kwa miezi sita ninaweza kusema nina furaha kuwepo hapa, kazi yangu ni kuhakikisha klabu inafanya vizuri ndani ya miezi sita, kuisaidia kupiga hatua zaidi, naelewa kuna  makocha wengi sana wangependa kuwa makocha wa Man U na mimi ni miongoni mwao lakini hilo si la kuliongelea sasa, bodi itafanya mchakato kumpata kocha wa kudumu miezi sita ijayo.

Mwandishi: Kuelekea dirisha la usajili la januari, unaionaje klabu?.

Ole Gunnar Solskjaer: Kwanza nahitaji kuwajua wachezaji wote, kuwaona. Nawajua, nilikuwa nikiwatazama wakati nipo Norway, lakini nahitaji kuwajua hasa, wapi niwaimarishe, kwahiyo siwezi kuzungumzia masuala ya usajili kwa sasa, kwakuwa kazi yangu ni kuwafanya wachezaji waliopo wacheze na wafurahie mpira.

Mwandishi: Kiwango cha Romelu Lukaku, kimeonekana kuwa vibaya, kwa mechi kadhaa. Unalizungumziaje hilo?

Ole Gunnar Solskjaer: Yaah kuna hilo na bado hatujaonana, hatujaonana pia na Alexis Sanchez nasikia yuko anakuja, kwahiyo nawatafuta ili tuyaweke sawa.

Mwandishi:Una masaa 24 tangu uwe kocha, unaionaje mechi yako ya kwanza dhidi ya Cardiff?

Ole Gunnar Solskjaer: Mimi kama kocha hii ni kazi yangu na nitakuwa hapa kwa msimu mzima, lakini kuna mechi nyingi sana, kwahiyo ni kitendo tu cha kupanga kikosi kitakachonipa ushindi na kila mchezaji inapaswa ajue akipata nafasi aweze kuitumia.

Mwandishi: Unadhani una nafasi gani ya kuifanya Man U ipunguze “gap” la alama na kufikia nafasi 4 za juu?

Ole Gunnar Solskjaer: Kwanza nafikiria kuhusu mechi yangu ya kwanza, pia kuwapa msingi wa uchezaji wachezaji na falsafa, nataka wajua napenda soka la aina gani kama timu, tutaangalia tutakusanya alama ngapi lakini kwa sasa nitatumia mbinu kutokana na mechi husika.

Mwandishi: Unaonaje kwako haitakuwa kama “tricky” kupanga timu ambayo wachezaji wake wanafikiria kuhusu kocha wa kudumu, hali wakijua wewe ni kocha wa muda tu, unadhani wataonyesha morari sawa?

Ole Gunnar Solskjaer: Kazi yangu ni kuwasaidia wachezaji, wawe vizuri kwakuwa wote watakuwa sehemu ya kikosi cha Man U hata baada ya kuja kwa kocha mpya, Mimi kama kocha ninajua jinsi ya kuishi na wachezaji, wamasiliano na nitaongea nao juu ya kile ninachotegemea kutoka kwao, unajua kama timu tumeweka vigezo vya kuwa hapa ni kimojawapo ni kuwa mchezaji wa timu, na naamini wachezaji wote watacheza, hakuna atakayebaki benchi isipokuwa mimi. Kwahiyo neno langu kwa wachezaji, watumie uwepo wangu kujisafishia njia kisoka na mimi pia.

Mwandishi: Ni kwa kiwango gani Sir Alex Ferguson anakushawishi kama kocha?

Ole Gunnar Solskjaer: Ferguson ana ushawishi wa kila kitu kwangu, napenda jinsi alivyokuwa anaishi na watu, jinsi anavyosimamia kikosi cha wachezaji 25 wa kimataifa. Pia hata bodi ya timu ni watu muhimu kwangu, nakumbuka hata 2003 nilivyokuwa majeruhi alionesha kunijali sana na kunifanyia vitu vingi (Ferguson).

Mwandishi: Umeifundisha Cardiff city je unadhani umeiva vyakutosha kama kocha, vipi mashabiki watarajie nini?

Ole Gunnar Solskjaer: Sanaaa! Kuifundisha Cardiff nimejifunza mambo mengi, nilifanya makosa kidogo, lakini kama hufanyi makosa huwezi kujifunza  lakini kwa sasa niko ligi kuu na sidhani kama yatajirudia hayo makosa.

Mwandishi: habari Ole! Umepata uzoefu mkubwa na jinsi ya kuishi na wachezaji, mchezaji kama Pogba utamfanyaje ili awe bora?

Ole Gunnar Solskjaer: Ni jukumu langu kumfanya kila mchezaji kuwa bora, tuko wote wakati wa mazoezi wanachohitaji ni kufundishwa  falsafa, misingi na aina ya uchezaji. Haijalishi unaifundisha timu gani au una wachezaji wa aina gani lakini kikubwa wachezaji inatakiwa wawe na taswira nzima ya jinsi unavyotaka wacheze, wachezaji wanatakiwa wajiamini katika kila mchezo.

     Huo ndio ulikuwa mwisho wa mkutano wa kwanza wa Ole na waandishi wa habari. Je unadhani kwa jinsi alivyojibu maswali kutoka kwa waandishi atakuwa ni kocha wa aina gani?


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.