Tetesi

Kocha mpya Yanga huyu hapa

Sambaza....

SIO Patrick Aussems tena kama wengi walivyoelekea kuamini mara baada ya taarifa kuibuka kwenye mitandao kuwa mabingwa wa Yanga wako kwenye hatua za mwisho kumuajiri kocha huyo wa zamani wa Simba.

Lakini ikufikie hapo ulipo taarifa mpya kwamba Yanga imebadili gia angani, ingawa sababu za kufanya hivyo, bado hazijafahamika na sasa klabu hiyo imeamua kuelekea nchini Hispania na kuibuka na jina la Angel Perez Lopez.

Aussems, aliyekuwa kocha wa Simba

Licha ya kuwepo taarifa kuwa Aussems kuwa miongoni mwa makocha walioomba kibarua kwenye klabu hiyo, lakini taarifa za uhakika ni kuwa wamevutiwa zaidi na wasifu wa Perez aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Getafe inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania.

Timu yake ya mwisho kufundisha ni timu ya Taifa ya Equatorial Guinea mwaka huu, ambapo pia kwa mujibu wa chanzo chetu amepata kufundisha timu mbalimbali.

“Inaonekana Mhispania tayari amekubalia, ni kijana mwenye umri mdogo na ana uwezo mkubwa katika kufundisha,” kilisema chanzo chetu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.