Mabingwa Afrika

Kocha Simba: Tumejiandaa lengo letu ni robo fainali

Sambaza....

Kuelekea mchezo wao wa tano wa Kundi C katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya kocha wa Simba ametema cheche akinyesha kujiamini katika kutimiza malengo yao.

Robert Oliveira amesema wamejiandaa vyema na lengo lao bado lipo palepale katika kufuzu robo fainali kutoke kundi lao lenye wababe Raja Casablanca ambao wameshafuzu tayari.

 

“Lengo letu ni moja kushinda na kuingia robo fainali, tunawaheshimu wapinzani wetu Horoya lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunashinda.

“Nawaamini wachezaji wangu, tumeweza kushinda mechi mbili nyumbani na ugenini dhidi ya Vipers na tumecheza vizuri pia hata kesho tutafanya hivyo siku zote mimi ni mtu chanya,” amesema Robertinho Oliveira.

Simba watakua dimbani leo kwa Mkapa saa moja jioni kuwakaribisha Horoya ya Guinea katika mchezo ambao Simba ni lazima washinde ili waweze kufuzu kwenda hatua ya robo fainali.

Kinara wa kundi Raja Casablanca yeye ana alama 12 akiwa ameshafuzu tayari, Simba wao wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama zao sita halafu wanafuata Horoya wenye alama nne na kibonde Vipers ana alama moja pekee.

Hivyo ili Simba afuzu ni lazima amfunge Horoya ambae ndio mshindani wake katika nafasi ya pili. Katika mchezo wa awali Horoya alipata ushindi wa bao moja kwa sifuri wakiwa nyumbani.

Simba wanapaswa kukumbuka jinsi walivyoifunga AS Vita na kutinga robo fainali mwaka 2019 na kutinga robo fainali wakipita katika kundi lao na Al Ahly. Ni wazi historia inawabeba Simba katika dimba la Benjamin Mkapa haswa katika mechi za maamuzi kama hizi.

Sambaza....