Kim Polsen
Mataifa Afrika

Kocha Stars: Tuna kibarua kizito mbele ya Algeria!

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa pili dhidi ya Algeria wa kundi F katika michezo wa kufuzu Afcon mwakani nchini Ivory Coast kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Kim Polsen amekiri wanakwenda kukutana na mtihani mzito.

Kim Polsen akiongea na waandishi kuelekea mchezo huo amesema ni wazi tunakwenda kukutana na miongoni mwa vigogo wa soka Barani Afrika.

“Algeria ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika, wana wachezaji wenye vipaji na uzoefu wa hali ya juu,” alisema Kim Polsen

Algeria

“Algeria huwa wana nafasi kubwa ya kushinda bila kujali wanacheza nyumbani kwao au ugenini. Utakua haupo sahihi kama utaipa nafasi kubwa Taifa Stars  kushinda mchezo mbele yao” Kim aliongeza.

Kocha Kim pia alisema wao kama benchi la ufundi wanajua ubora wa Algeria na wanajiandaa vyakutosha ili kwenda kuwa washindani na kupata matokeo mazuri.

“Mimi na kocha wangu msaidizi Shadrack (Nsajigwa) tupo makini kuelekea mchezo huo mgumu. Tumewaambia wachezaji wapunguze makosa kwasababu katika hatua hii waliyopo kosa dogo sana linaweza kukuadhibu,”

“Mchezo utakua mzuri tunacheza na timu ngumu lakini pia nasisi ni washindani hivyo haitakua rahisi na hautakua mchezo mwepesi,” Kim Polsen

Katika mchezo wa kwanza wa Algeria walifanikiwa kuifunga Uganda  mabao mawili kwa bila huku pia wakitawala mchezo kwa kiasi kikubwa.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.