Ligi

Kocha wa Simba amtamani Golikipa wa KMC

Sambaza kwa marafiki....

Jana kulikuwa na mchezo Kati ya KMC na Simba katika uwanja wa uhuru , mechi ambayo ilimalizika kwa Simba kushinda goli 2-0 na kuzidi kujikita kileleni kwa jumla ya alama 21.

 

Baada ya mchezo huo kocha wa Simba alisema kuwa timu yake haikucheza vizuri hasa hasa kipindi cha kwanza , lakini kipindi cha pili ilicheza vizuri na kufanikiwa kupata magoli mawili.

Kuhusu uwezekano wa kufunga magoli zaidi ya mawili kocha huyo alidai kuwa Simba walikuwa wanauwezo wa kufunga zaidi ya magoli 2 lakini golikipa alifanya kazi nzuri.

“Tulistahili kufunga magoli zaidi ya mawili , lakini golikipa wa KMC aliwasaidia, alifanikiwa kufanya saves zaidi ya nne ambazo zilikuwa ni goli”.

Kuhusu kiwango cha timu ya KMC kocha huyo alidai kuwa timu hiyo ina kiwango kikubwa na hastahili kuwepo hapo. “Timu inacheza vizuri sana , na hastahili kuwepo kwenye nafasi waliyopo kwa sasa kwenye ligi kuu” alidai kocha huyo ambaye mpaka sasa hivi amecheza mechi 3 akifanikiwa kufunga magoli 12 huku akiwa hajafungwa hata goli moja. Unakionaje kiwango cha kocha huyo ?

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.