Wydad Casablanca wapinzani wa Simba katika robo fainali
Uhamisho

Kocha wa Simba Apewa Kazi Wydad Casablanca

Sambaza....

Wababe wa Simba katika Ligi ya Mabingwa Wydad Cadablanca wamemtimua kocha wake Juan Carlos Garrido na kuamua kuamua kumpa kibarua kocha wa zamani wa Simba.

Baada ya kumtimua Garrido Wydad wamemtambulisha rasmi Sven Vandebroeck aliyekua kocha wa Simba na tayari ameshaungana na Wamorroco hao katika uwanja wa mazoezi.

Kocha Sven Vandebroeck akiwa mazoezini Wydad Casablanca.

Sven ambae aliiongoza Simba mwaka 2019 mpaka 2021 na kuicha Simba ikiwa imeshafuzu hatua ya makundi anaikuta Wydad Casablanca ikiwa tayari nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa  Afrika lakini pia katika Ligi inashika nafasi ya pili wakiwa na alama 50 wakiachwa alama moja na AS FAR vinara.

Sasa Mbelgiji huyo anakibarua chakutetea taji la Ligi ya Mabingwa Afrika lakini pia na taji la Ligi Kuu ya Morocco Batola Pro ili kukifanya kibarua chake kua salama zaidi.

 

 

Sambaza....