Sambaza....

Kocha wa zamani wa Chelsea, Steve Clarke ameishauri timu yake kufikiria kumuuza mshambulijai wao Eden Hazard ili kupata fedha za kutumia kununua wachezaji wengine katika usajili wa majira ya joto.

Akizungumza na kipindi cha redio cha Shirika la utangazaji la Uingereza BBC, Clarke ambaye alikuwa kocha msaidizi kwa kipindi cha miaka minne (2004-2008) amesema Chelsea wanapaswa kujifikiria upya wakati wa kufanya usajili ikiwezekana kutumia pesa nyingi kama vilabu vingine ili kujiimarisha msimu ujao.

Steve Clarke

“Unaona namna ambavyo Manchester United na Manchester City wanavyotumia pesa na inafanikiwa, kama tunafikiria kuwa juu lazima tufanye kama wao, lakini ndani ya uwezo kama inawezekana, nina uhakika bodi itafanya vile ambavyo inatakiwa kufanya,” amesema Clarke

Beki huyo wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Kilmarnock ambayo inashiriki ligi kuu ya  Scotland amesema haoni kama itakuwa rahisi kwa Chelsea kumuachia Eden Hazard kipindi hiki lakini ni muhimu kufanya hivyo.

“Siku zote tunaangalia namna unavyoweza kupata mbadala wa wachezaji, wanakuja na kuondoka, ila klabu ni kitu muhimu zaidi, Chelsea wanatakiwa kukijenga kikosi chao, wanakazi kubwa ya kufanya kipindi cha majira ya joto, ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya usajili wa wachezaji wengine ni lazima wamuuze Hazard,” Clarke amesema.

Ubingwa wa FA

Ikumbukwe Eden Hazard mwenye umri wa miaka 27, ndiye aliyefunga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya chama cha soka England dhidi ya Chelsea hapo jana katika uwanja wa Wembley jijini London, na amebakiwa na miaka miwili mkataba wake kufikia tamati.

Hazard akishangilia

Wakati hayo yakiendelea mlinda mlango wa klabu hiyo Thibaut Courtois naye ametoa ushauri kwa bodi ya Chelsea kuimarisha kikosi hicho ili kiwe na ushindani msimu ujao huku akitishia kuwapo katika kikosi hicho msimu ujao.

“Tutaangalia baada ya michuano ya kombe la dunia kama nitaendelea kuwepo ndani ya kikosi cha Chelsea ama laa” amesema Courtois mwenye umri wa miaka 26.

Sambaza....