Kocha msaidizi wa Yanga Cedric Kaze (katikati), Deus Kaseke (kulia) na Karim Boimanda Afisa habari wa bodi ya Ligi(kushoto)
Blog

Kocha Yanga: Ratiba ni Ngumu Lakini Tutafikia Malengo

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga na Kagera Sugar kocha na kiungo wa timy hiyo wametema cheche walipokua wakiongelea mchezo huo mbele ya Waandishi wa habari

Denis Nkane aliyeongea kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema malengo yao yapo palepale yakutwaa ubingwa na wapo tayari kufanya vyema kuelekea katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Kagera Sugar.

 

“Sisi kama wachezaji tunajua umuhimu wa mechi ya kesho haswa katika kujihakikishia malengo yetu ya kuchukua ubingwa, tuna imani tutafanya vizuri na tutapata alama tatu mbele ya Kagera Sugar,” alisema Denis Nkane

Nae kocha wa Yanga Cedrik Kaze amesema ratiba kwa upande wao ni ngumu mno lakini hawana namna zaidi ya kujiandaa na kupata matokeo mazuri katika kila mchezo.

Cedrick Kaze “Changamoto kubwa ambayo ipo ni ratiba tuliyonayo, mechi zinakaribiana sana. Tazama tuna mechi za Kimataifa, mechi za Ligi Kuu na FA. Lakini pia mbali na hayo sisi benchi la ufundi tunawaanda wachezaji wetu vizuri kupata matokeo mazuri katika kila mchezo uliopo mbele yetu.”

Yanga wana kibarua kigumu kesho katika Dimba la Azam Complex majira ya saa mbili usiku mbele ya Kagera Sugar ambao katika mchezo wa awali Wananchi waliibuka na ushindi wa bao moja sifuri.

Sambaza....