Tahariri

Kongole kwa Wananchi!

Sambaza....

Felicidades Wananchi, Toutes nos félicitations Wananchi, Congratulazioni Wananchi, Hongera Wananchi. Hizi ni lugha zaidi ya nne zikiwa na maana ya kuwapongeza Yanga.

Hii sio kwa bahati mbaya kutumia lugha zote hizo sio kwamba n nimekosea ila ni kuonyesha msisitizo kwani najua mwanzo wa safari yetu na kila usafiri milio tumia  naufahamu.

Mlitumia nyundo kwenye kuuwa sisimizi, hapa naitazama safari yenu dhidi ya Zaalan fc kutoka Sudan Kusini hii ili kuwa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, goli tisa dhidi yao  zikawapa matumaini mapya katika klabu bingwa.

Djuma Shaban akipiga kross mbele ya mchezaji wa Zaalan Fc katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Lakini haikuwa kwenye safari yenu yapili dhidi ya ndugu zao tena kutoka Sudani hapa namanisha Al Hilal, mlipanda ndege wakati Passport mmesahau Jangwani mlipo zirejea mkajikuta safari yenu imeishia hapo.

Mkahamia upande wa pili wa shilingi na mkadondokea kwenye kombe la Shirikisho Afrika na ratiba kutoka kila mtu akaongea lake na walio wapenda wakawakumbusha kuwa safari hii msisahau Passport zenu Jangwani.

Mwongoza njia Nasrdin Nabi  yeye ndie pekee alikuwa anajua ni njia gani anawapitisha japo ilikuwa na miba lakini mkapita salama kwa suluhu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na goli la Mburkinabe Stephan Azizi ki likafufua matumaini ya Wananchi kufika katika nchi ya ahadi.

Aziz Ki mfungaji wa bao pekee la Yanga nchini Tunisia

Kila mtu aliamini safari ya Wananchi itaishi uwanja wa ndege wa Mwalim Julius Kambarage Nyerere pale makundi yalipopangwa tu, hapa namaanisha kundi lenu likiwa na timu kama US Monastir, Tp Mazembe na Real De Bamako lakini bado kiongozi wa safari yenu na shujaa wenu alikuwa anajua wapi anawapeleka.

Makundi yakatamatika mkiwa mnaongoza kundi lenu tena mkimfunga Tp Mazembe nje ndani na hapa  ndio ile safari yenu ya kwenda nchi ya ahadi ikiwa na vikwazo kadhaa lakini hamkukata tamaa na mkapambana mpaka mkafanikiwa.

Nchi inaingia kwenye historia, kwa mara ya kwanza timu kutoka Tanzania inatinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho huku wenyewe mkiwa hata hamringi na mambo yanawaendea tu. Hapa kuna lakujifunza kutoka kwenu nakwenda kwa timu nyingine hapa nchini kwani namini hata nyinyi mlijifunza kutoka kwa mtani wenu alieyefanikiwa kufika robo fainali Klabu Bingwa Afrika mara 3 katika miaka mitano aliyoshiriki kombe hilo.

Yanga Sc “Wananchi”

Ila nyuma ya hayo yote nyota na rubani wa safari yenu ya matumaini yakuelekea nchi ya ahadi ni Injinia Hersi Said akiwa kama Rais wa timu. Wacha niishie hapa maana nina mengi juu yenu ila niseme tu “Siyakuhalalisela” ahhh kumbe nimeongea Kizulu acha niseme hongereni sana wananchi mimi sina ninacho wadai japo mna nafasi ya kuipigania bendera ya nchi.

Imendaliwa na Mwakyoma jr

Sambaza....