EPL

Kuelekea mechi na Palace, Ole amjaza upepo Fred.

Sambaza kwa marafiki....

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema anafikiria kumuanzisha kiungo wa kibrazil Frederico Rodrigues de Paula Santos maarufu kama Fred katika mchezo wa ligi ya England dhidi ya Crystal Palace usiku wa leo.

Solskjaer amesema ni wakati muafaka sasa kwa Fred kuonesha ubora wake kwani toka asajiliwe mwezi Juni mwaka jana amekuwa hapati nafasi kutokana na wachezaji Ande Herrera, Nemanja Matic na Paul Pogba kuonesha muunganiko mzuri.

Kutokana na kuumia kwao, Solskjaer ambaye toka achaguliwe kuwa kocha wa muda wa Manchester United amemuanzisha mara moja pekee na kama atamuanzisha katika mchezo wa leo basi itakuwa ndio mara yake ya pili kwa kiungo huyo ambaye anashika nafasi ya tano kwa wachezaji waliowahi kusajiliwa kwa bei kubwa na klabu hiyo.

“Fred anahitaji kupata muda wa kucheza, na anatakiwa kucheza vizuri pale anapopata muda, pia kufanya juhudi kwenye mazoezi, nina uhakika Freda atakapopata nafasi basi ataitumia vizuri, labda kwenye mchezo dhidi ya Palace, tumekuwa na viuongo watatu Pogba, Matic na Herrera wamecheza vizuri pamoja,” Solskjaer amesema.

Manchester United wameondolewa kwenye nafasi ya nne baada ya kutoka sare dhidi ya Liverpool hivyo watahitaji ushindi kwenye mchezo huu wa leo ili kurudisha matumaini ya kuendelea kubaki kwenye nafasi ya nne za juu kwenye ligi hiyo pendwa zaidi duniani.

“Vita ya nafasi nne za juu inavutia na itaendelea kuvutia, bado kuna michezo mingi mbele yetu mpaka kufikia mwishoni mwa ligi, na ukiangalia hakuna tofauti kubwa ya alama kwa timu zinazoshika nafasi ya nne, tano na sita,” Solskjaer amesema.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.