Kelvin John Kushoto
Blog

Kelvin John- Licha ya kupoteza, tumejifunza vingi.

Sambaza kwa marafiki....

Tovuti ya kandanda.co.tz kwa wiki hii yote itakuletea mahojiano ambayo imefanya na Kelvin John, mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys). Fuatilia mfululizo wa mahojiano hayo kwa njia ya uchambuzi pekee hapa hapa katika ulimwengu wa soka, ukiletwa na mimiMartin Kiyumbi.


1- Mechi za kirafiki hazikutujenga – Kelvin John (1)


Baada ya michuano ya AFCON kumalizika, ambayo ilikuwa ikifanyika kwa mara yackwanza nchini Tanzania, Kelvin John anakiri licha ya matokeo mabaya bado aliweza kujifunza kitu.

Akiongea na kandanda.co.tz, Kelvin John ametuambia alijifunza vitu vingi sana.

“Kuna vitu vingi ambavyo nimejifunza , pamoja na kwamba timu yetu haijafanya vizuri ila mimi binafsi kuna vitu vingi sana nimejifunza kwenye michuano hii ya Afcon.” -Kelvin John.S

Timu inapokuwa na matokeo tofauti uwanjani au hata inapotafuta ushindi, mazungumzo au maelekezo kutoka kwa benchi la ufundi. Lakini pia nahodha na wachezaji au wachezaji wenyewe uwanjani ni muhimu kuzungumza na kujadiliana kupata ufumbuzi au kuongeza morali.

Kelvin tulijaribu kuumuliza pia kumdadisi zaidi na akafunguka pia kipi zaidi alijifunza.

“Aaaah vingi , kwa mfano kama uliangalia mechi yetu dhidi ya Nigeria wakati tunaongoza wachezaji wa Nigeria waliitana kwa pamoja.

Tanzania vs Nigeria

Kama mnakumbuka katika mechi hii, Nigeria walipata nguvu zaidi na kuanza kushambulia lango la Serengeti Boys.

“Baada ya kuitana waliamua kila mmoja aanze kucheza kwa uwezo wake binafsi ili kuisaidia timu yao kupata matokeo.” Kelvin

Kitu hiki hata benchi la ufundi la Serengeti hawakujua nini cha kufanya. Kwakuwa mpango wao ulifanikiwa na kuwezesha Nigeria kushinda. Kwa upande wa Kelvin anasema “Hii ilikuwa tofauti na kwenye timu yetu ambapo tuliendelea kucheza kwenye mfumo ule ule ambao alituelekeza kocha.”

Mwalimu pamoja na benchi lake ni muhimu kujua haya mapema, na bila shaka ni fundisho pia kwa timu zetu kujifunza kujiongeza uwanjani pindi mambo yanapokuwa tofauti.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.