Ligi Kuu

Lyanga mkali wa rekodi Coastal Union!

Sambaza....

Mshambuliaji wa Coastal Union na timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Ayoub Lyanga amezidi kuonyesha yeye ndie mchezaji muhimu katika klabu ya Coastal Union baada ya kila siku kuendelea kuandika rekodi nzuri katika  katika Ligi Kuu Bara.

Lyanga amekua mchezaji muhimu na wakutumainiwa katika klabu yake ya Coastal na kuweza kusiadia kushika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na alama 46 tofauti na msimu uliopita ambapo kipindi kama hiki Coastal ilikua ni miongoni mwa timu zinazopambana ili zisishuke daraja.

Ayoub Lyanga akipambana na Aron Lulambo “Makoena” katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Namba hazidanganyi Ayoub Lyanga mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao 7 huku pia akitoka msaada wa bao “assist” mara 5 na hivyo kumfanya kua kinara katika klabu yake ya Coastal Union katika kuhusika na mabao.

Ayoub Lyanga mchezaji wa zamani wa Zanaco ya Zambia na ndugu wa damu kabisa wa Danny Lyanga mshambuliaji wa JKT Tanzania pia anasifikia katika kupiga mipira iliyokufa na kuweza kutengeneza mabao ama msaada wa goli.

Tazama hapa rekodi zake akiwa na Klabu yake ya Coastal Union.

Takwimu za Ayoub Lyanga akiwa na Coastal Union.

Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.