Ligi

MA REFA wanashinikizwa kuionea YANGA-Mkwasa

Sambaza....

Jana kulikuwa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara Kati ya Mbeya City na Yanga. Mchezo ambao ulikuwa wa kiporo na tulishuhudia Yanga ikilazimishwa Suluhu na Mbeya City iliyochini ya Amri Said.

Kocha huyo mpya aliyekuja kuchukua nafasi ya Juma Mwambusi , alisema kwa sasa amefurahia na namna ambavyo timu yake inacheza. “Tumepata point moja , Yanga nao wamepata point moja na point nyingine wameichukua TFF”.

“Nina furahia jinsi wachezaji wangu walivyopambana hivo kikosi chetu kinazidi kuimarika Siku Baada ya siku”-alisema kocha huyo wa zamani wa Biashara United na Mbao FC ya Mwanza.

Kwa upande wa kocha wa muda wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amedai kuwa hali ya uwanja ilikuwa Mbaya . “Hali ya uwanja ilikuwa mbaya , uwanja ulijaa maji wachezaji wakawa wanakosa timing ndani ya uwanja”.

Kuhusu waamuzi , kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” amedai kuwa kwa sasa waamumizi wanachezesha kwa kushinikizwa.

“Waamuzi wamefanya maamuzi ambayo wachezaji hawajaridhishwa nayo hata mashabiki walionekana kutoridhishwa nayo , waamuzi wasichezeshe kwa kushinikizwa , waamumizi ni kichefu chefu na kama tukiendelea hivi hatutoendelea ” alimalizia kocha huyo.

Yanga itasubiri kucheza tena Siku ya tarehe 27 dhidi ya Prisons FC Katika uwanja huo huo wa Sokoine mjini Mbeya ikiwa ni katika kumalizia viporo vyake.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x