Ligi Kuu

Makosa ya kibiashara kwa wachezaji wetu

Sambaza....

Sote tunamapenzi ya vilabu kadhaa wa kadhaa vya mpira wa miguu, na kuna wakati mwingine tunaweza jisahau na kutokea tukiwa na jezi zetu. Stori za ukweli zipo nyingi, wapo watu wamefanya kazi kiwanda cha coca cola lakini kinywaji chao pendwa ni pepsi cola, wengine hawajawahi kunywa bia za Serengeti lakini wakajikuta wakifanya kazi katika kiwanda hicho na tujuavyo mnywaji bia hu’fall in love’ na aina moja au mbili tu za kinywaji, hapo sijawagusa wavuta sigara.

Mkanganyiko huu siku zote unaamuliwa na kitu kinaitwa Kanuni za Maadili au ‘Code of Conducts’ au Ethics, hapo ndipo huruhusiwi kuvaa jezi ya Tigo ukiwa katika ofisi za Vodacom au Fulana ya Chadema katika Mkutano wa CCM, lakini iwapo tu kuna lengo linatakiwa kutimizwa.

Mtandao wetu umekukusanyia mambo kumbi ambayo tunadhani wachezaji au timu zetu zinafanya makosa.

1 Kuvaa katika kadamnasi jezi za timu nyingine

Wachezaji ni vyema wakavaa jezi au fulana zenye nembo za timu husika wanapokuwa katika maisha ya kawaida, au wavae mavazi ambayo hayana nembo zozote.

2 Kutokea katika ‘interview’ bila mavazi ya timu

Katika mahojiano yoyote, iwe katika radio na zaidi yale ambayo yanaweza zalisha picha au video, wachezaji ni vyema wawe katika jezi au nguo zenye nembo ya timu husika.

3 Kukabidhiwa zawadi wakiwa na mavazi ya mtoa zawadi

Kumekuwa na utaratibu mara nyingi sana wachezaji au benchi la ufundi la klabu kupokea zawadi kutoka kwa wadhamini au watu ambao wameguswa na timu au mchezaji katika matokeo au kama shukrani. Ikumbukwe musika anapopokea zawadi hapokei yeye kama binafasi, bali ni kama mfanyakazi wa klabu husika. Mtandao wetu umekuwa ukitoa zawadi kwa wafungaji bora kila mwezi, tumegundua umuhimu wa wahusika kuwa katika jezi za timu zao wakati tunawakabidhi.

4 Kusahau kuongelea kuhusu timu yake

Wachezaji hujisahau wanapoulizwa kuhusu masuala ya klabu na kuanza kuongelea zaidi kuhusu klabu nyingine.

5 Kutoa taarifa za klabu bila idhini ya klabu

Ramadhani Kabwili

Hivi karibuni golikipa wa Yanga SC, Kabwili alitoa tuhuma nzito sana kuhusu upangwaji matokeo akihusisha klabu ya Simba. Katika taratibu za kuongea na vyombo vya habari anatakiwa kuwa muangalifu, na pia kuwasiliana na uongozi nini cha kuongea.[su_spoiler title=”Kabwili”]Kabwili hajaonekana kuidakia klabu hiyo kwa kipindi kirefu sasa.[/su_spoiler]

Ongezea na yako pia utupe maoni yako


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.