Blog

Manara ana “UONGO” mtamu

Sambaza....

Hapana shaka mapigo ya moyo wa Tanzania siku ya Jumapili yalisimama ghafla. Hayakuweza kuendelea kutembea hata kwa dakika moja kwa sababu ya maumivu.

Maumivu makubwa, maumivu ambayo hayakutegemewa kabisa kuwepo kwa siku ya jana. Wengi hawakutegemea kupata maumivu kwa jana.

Mategemeo yalikuwa makubwa mno, na kama ujuavyo mategemeo makubwa siku zote huumiza mioyo ya wengi.

Hiki ndicho kitu ambacho kilitokea kwa jana. Nani alitegemea Simba jana kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika?

Timu ambayo msimu uliopita ilifika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika? tena ikiwa na wana fainali wa michuano ya vilabu barani Afrika msimu juzi ?

Achana na Alhly ambao msimu juzi walifanikiwa kufika fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Simba walipangwa kundi moja na As Vita pia ambao msimu juzi walifika hatua ya fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Huu ulikuwa mlima mrefu sana, mlima ambao wengi waliona Simba hawataweza kuupanda tena, lakini cha kushangaza timu zote zilikuwa zimepangwa na Simba kundi moja zilifungwa kwenye uwanja wa Taifa.

Uwanja ambao wengi waliamini ni uwanja mgumu kwa timu yoyote ile ambayo ingekutana na Simba , lazima ingeacha alama tatu kwenye uwanja huo.

Hapo ndipo ujasiri wa Simba kufanya vizuri kwenye michuano hii ulianza. Wengi waliona Simba wanaelekea sehemu ambayo kina TP Mazembe wameshatangulia.

Hakuna ambaye alikuwa na uhakika wa kwenda kupata hata sare kwenye uwanja wa Taifa mbele ya Simba. Ndiyo maana tuliamini UD Songo hatoweza kupita kwenye michuano hii.

Asingeweza kufanya chochote mbele ya Simba , ikizingatia na usajili ambao waliufanya ilikuwa ngumu kuamini Simba wangetolewa tena kwa goli la ugenini lililopatikana kwao.

Waliumia sana, walilia sana, Taifa lilisimama kwa muda kuomboleza kilio hiki, kilio ambacho kabla ya kutokea tuliaminishwa na Haji Manara kuwa tuna wanajeshi ambao wangefika nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x