Sure Boy akimuacha kiungo wa KMC Abdul Hillal
Blog

Manara na Zaka wanatafuta KIKI kupitia YANGA

Sambaza....

Jana Azam FC kupitia kwa mkuu wa kitengo cha habari cha Azam FC , Zaka za Zakazi walielezea kitu ambacho wao wamekiona kama uhuni unaofanywa na Yanga.

Zaka za Zakazi alidai kuwa wakati Yanga wanaleta barua ya kumtaka Salum Abubakary “SureBoy” walimtuma mwanachama wa Yanga kitu ambacho ni kizuri.

Lakini jana mwanachama huyo huyo alileta barua ya Salum Abubakary “SureBoy” ya kuomba aondoke katika klabu hiyo. Zaka Za Zakazi amedai kuwa barua hiyo imekanwa na Salum Abubakary “SureBoy”.

Zaka za Zakazi alidai kuwa kitendo hicho siyo kizuri na kinafanywa na klabu kubwa na yenye heshima kubwa hapa nchini. Hawastahili kuandika barua na kujifanya ni mchezaji na kutuletea sisi.

Zaka za Zakazi aliwataka Yanga watoke hadharani na watuambie kwanini wamegushi barua hii na waombe radhi kwa kitendo walichokifanya tofauti na hapo watalifikisha jambo hili sehemu nyingine.

Salum Aboubakar “Sure boy” akimtoka mchezaji wa Ruvu Shooting

Baada ya jana Zaka Za Zakazi kuongea hivo leo hii Afisa Habari wa Yanga , Hassan Bumbuli amedai kuwa wasemaji wengi wa vilabu wamekuwa wakiisema Yanga ili wapate kiki na followers mtandaoni.

“Kuna kitendo kimeanza kuonekana kuwa wasemaji wengi wa vilabu hapa nchini wanaisema Yanga ili wapate Kiki . Hata upande wa pili msemaji wao haiwezi kupita siku bila kuisema Yanga”.

“Kuisema Yanga ndiyo kula kwake , bila kuisema Yanga hali. Wanaisema Yanga ili wapate followers mtandaoni. Hii tabia tunataka kuikomesha”. Alisema Hassan Bumbuli.

“Tunataka kuanzia kesho Zaka Za Zakazi atoke mbele ya umma na aseme ni mtu gani wa Yanga aliyeleta barua na ataje ID number ya huyo mtu na ataje kuwa ametoka katika ofisi gani ya Yanga”- alimalizia Hassan Bumbuki


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.