EPL

Manchester city yajawa na matumaini ya kunasa saini ya Ronaldo.

Sambaza kwa marafiki....

Klabu ya soka ya Manchester City ya England imepata matumaini ya kumsajili kinda wa Benfica ya Ureno Ronaldo Camara ambaye anawaniwa na vilabu vingine vikubwa ikiwemo Barcelona na Manchester United.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 16 ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa tishio katika siku za usoni kwani tayari amekuwa katika rada za vilabu vikubwa na tayari maskauti kutoka Old Trafford na Nou Camp walishatumwa kwenda kumuangalia.

Lakini Manchester City wamekuwa karibu zaidi wakifuatilia mwenendo wa kinda huyo na matumaini yao ni kuona anajiunga mapema kwenye kituo cha kukuza vipaji cha klabu hiyo na kuwa karibu zaidi na kocha Pep Guardiola kabla ya kuangalia utaratibu wa kumsajili.

Camara ni mchezaji anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na amekuwa akiitumikia timu ya taifa ya Ureno ya chini ya umri wa miaka 17, na kama atajiunga na Manchester City basi atakuwa anatimiza ndoto za klabu hiyo za kuwa na mchezaji ambaye hapo baadae atakuja kwa star wa dunia.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.