Tetesi

Mbappe kuondoka PSG, United waangukia kwa Duncan Rice

Sambaza....

Tetesi za soka zilizotawala na kugonga vichwa vya habari katika magazeti mbalimbali Barani Ulaya leo hii!

Mshambuliaji Kylian Mbappe amebakisha mwaka mmoja pekee katika mkataba wake na PSG wanataka kumuongezea mwaja mmoja zaidi ili asije akaondoka bure. PSG wanataka kuongeza mkataba wa Mbappe si kwa kumzuia kuondoka lakini wakitaka kuumuza kwa hela nyingi kwenda Madrid.

United wanaamini watapata saini ya kiungo wa West Ham Duncan Rice licha ya nyota huyo kuonyesha kutamani kuendelea kubaki katika Jiji la London. Arsenal pia imetajwa kumuhitaji nyota huyo wa timu ya Taifa ya England.

Chelsea huenda ikaamua kumrudisha mshambuliaji wake wa zamani Tammy Abraham katika usajili wa dirisha kubwa kutoka AS Roma. Kuna kipengele cha kumrudisha nyota wao huyo kwa ada ya pauni milion 70 baada ya misimu miwili kumalizika.

Arsenal na Newcastle wapo tayari kupambania saini ya kiungo Mbrazil wa West Ham Lucas Paqueta. West Ham ipo tayari kumuachia nyota huyo kwa ada ya pauni milioni 62 tu.

Sofyan Amrabat

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema anahitaji kusajili angalau viungo watatu au wanne wapya ili kuweza kuendelea kushindana England na Ulaya. Miongoni mwa nyota anaowahitaji ni pamoja na Jude Bellingham wa Dortmund, Sofyan Amrabat wa Fiorentina na Moises Caicedo wa Brighton.

Sambaza....