Kotei (Kushoto) akimthibiti Muleka wa TP Mazembe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ambao uliisha kwa sare
BlogMabingwa Afrika

Mchezo wa TP Mazembe wahairishwa, kumuua Mnyama.

Sambaza....

Wakati shirikisho la soka nchini TFF likiuhairisha mchezo kati ya Simba na Biashara United uliotakiwa kuchezwa siku ya jumatano katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, kule nchini Congo, TP Mazembe nao walitakiwa kucheza siku ya jana dhidi ya Maniema Union lakini mechi hiyo nayo imehairishwa.

Sababu kuu za kuhairishwa kwa mchezo huo katika ligi kuu nchini Congo inayojulikana kwa jina la Linafoot, ni maandalizi ya TP Mazembe kuelekea mchezo wao wa marudio dhidi ya Simba Sc ya Tanzania katika mashindano ya klabu bingwa Afrika.

Mchezo huo ulioahirishwa, ni dhidi ya Maniema Union inayoshika nafasi ya 4 katika msimamamo wa Linafoot ikiwa na alama 54, na katika mchezo huo TP Mazembe wangekuwa ugenini.

Katika mchezo wa awali TP  Mazembe walipata sare ya kutofungana  ugenini, na sasa chama cha Soka nchini humo kimewapa muda zaidi wa kujiandaa na mchezo wa marudiano ili kuhakikisha klabu hiyo inasonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

TP Mazembe chini ya kocha Pamhile Mihayo Kazembe, inashika nafasi ya  2 katika msimamo wa Linafoot ikiwa na alama 58 wakicheza michezo 23 nyuma ya vinara AS Club Vita wenye alama 65 katika nafasi ya kwanza wakicheza michezo 25.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x