Benard Morrison akishangilia goli lake la kwanza akiwa na jezi ya Simba, pamoja na kiungo Said Ndemla
Ligi Kuu

Mechi mbili za Morrison bila goli , assist , bila kucheza vizuri !

Sambaza....

Moja ya usajili ambao ulishika habari kwenye vyombo vya habari hapa nchini ni usajili wa Bernard Morrison. Usajili huu ulikuwa na vute ni kuvute kutoka kwa miamba wawili wa mpira nchini Yanga na Simba.

Yanga walikuwa wanadai wana mkataba wa miaka miwili na Bernard Morrison , Bernard Morrison alidai kuwa hana mkataba na Yanga. Hivo kesi hii ilisikilizwa kwa siku tatu na maamuzi yakatoka kuwa Bernard Morrison hakuwa na mkataba na Yanga.

Bwalya, Mugalu, Mkude na Morisson

Rasmi akawa ameenda Simba. Moja ya kitu ambacho wengi walikuwa wanategemea ni kuona moto wa Bernard Morrison. Moto ambao alianza kuuonesha akiwa Yanga.

Ligi imeshaanza mpaka sasa tupo katika mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara. Katika mechi hizi mbili Bernard Morrison ameonesha kiwango cha kawaida tofauti na tulivyokuwa tunadhania.

Najua bado mapema sana lakini kwenye mechi hizi mbili alizocheza kuna maeneo mawili ambayo hajafanikiwa sana ndani ya kikosi. Tuyatazame hayo maeneo mawili.

1: KUZUIA

Moja ya sifa kubwa ya mchezaji wa kisasa ni kuisaidia timu wakati timu ikiwa na mpira na wakati ambao timu haina mpira.

Bernard Morrison amekuwa mzuri sana kipindi ambacho timu ikiwa ina mpira tofauti na kipindi ambacho timu haina mpira.

Mohamed Hussein “Tshabalala” amekuwa hana msaada kipindi ambacho timu ikiwa inahitaji kujizuia kwa sababu Bernard Morrison haishuki kuisaidia timu kuzuia.

Mohamed Hussein “Tshabalala”

2: KUSHAMBULIA

Hili ni eneo ambalo Bernard Morrison analipenda na ndiyo eneo ambalo unaweza kuona ubora wake kuliko eneo jingine lolote.

Lakini ndani ya mechi hizi mbili hajaonesha ubora wake katika eneo hili. Hajafanikiwa kufunga , kutengeneza nafasi ya goli kama ambavyo tumezoea kutoka kwake.

KIPI AFANYE BERNARD MORRISON?

Najua wakati anakuja Simba mashabiki wengi wa Simba walikuwa wana mategemeo makubwa ya kiwango chake.

Ile presha kubwa kutoka kwa mashabiki ndiyo inayompa wakati mgumu Bernard Morrison kwa sababu wakati wote anawaza namna ya kufikia matamanio ambayo mashabiki wa Simba wanayatamani kutoka kwake.

Kingine Bernard Morrison anawaza namna ambavyo anaweza kuwanyamazisha mashabiki wa Yanga. Vitu hivi viwili anatakiwa kuachana navyo.

Maisha ya nje ya uwanja hatakiwi kuyaendekeza kwa sasa. Akili yake iwe ndani ya uwanja muda mwingi kuliko nje ya uwanja. Awaze namna ambavyo anaweza kufanya vyema aondokane na presha ya nje ya uwanja.

Sambaza....