Blog

Mgahawa Cafe kudhamini Galacha wa Magoli wa Kandanda

Sambaza....

Baada ya mafanikio makubwa ya mtandao wa habari, uchambuzi na takwimu za mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania, Kandanda (Tovuti na App), katika kusheherekea kila mwezi na aliyefunga mabao mengi zaidi, Mgahawa wa Mgahawa Cafe & Restaurant umevutiwa kudhamini kipengele hicho kwa msimu wa mwaka 2019/20.

Mgahawa huu ambao unapatikana Posta katika jengo la Golden Jubilee na Azura pale mikocheni, umeamua kuwa sehemu ya wadau wa michezo hususani mpira wa miguu kupitia tunzo hizi.

Mfungaji bora wa Ligi Kuu 2017/18

Ikumbukwe zawadi hizi zimekuwa zikitolewa kama njia ya kusheherekea mafanikio ya mchezaji katika upachikaji wa mabao pekee. Mchezaji wa kwanza kukabidhiwa zawadi hii alikuwa ni Eliud Ambokile (Aliyekuwa Mbeya City Fc), alifuatiwa na Meddie Kagere (Simba Sc), Emmanuel Okwi (Simba Sc), Heritier Makambo (Yanga Sc) na Salimu Aiyee (Akiwa Mwadui) hawa kwa uchache wake.


Wafungaji bora Agosti-Septemba


Mtandao wa Kandanda pia husheherekea mafanikio ya mfungaji wa jumla wa Ligi Kuu Tanzania bara, msimu uliopita alikuwa ni Meddie Kagere ambaye alipachika mabao 23 na kuwa Galacha wa Mabao wa Kandanda Ligi Kuu



“Tumeangalia kitu gani mchezaji anaweza kupewa kama zawadi na kikatumika kama motisha na kitendea kazi pia, hivyo tumekubaliana zawadi ya jozi moja ya viatu vya mpira” alisema Martin Kiyumbi, Msimamzi wa mtandao wa Kandanda uliochini ya kampuni ya Galacha.

Katika kuboresha sehemu hii ya zawadi, sasa kila mwezi mchezaji ambaye atakuwa amefunga magoli mengi zaidi kwa mwezi husika atapewa zawadi ya kiatu imara cha mpira wa miguu kikiwa kimeandikwa jina lake.

“Hatapata kiatu tu, akiwa yeye na mpenzi wake au mwenza au rafiki watapata free Dinner (Mlo wa usiku) katika Mgahawa wetu kwa siku moja tu” Bi Fatma Dahir, mkurugenzi wa Mgahawa Cafe and Restaurant aliongeza.

Utaratibu wa zawadi hizi utaanza rasmi mwezi Septemba, ambapo tutaangalia mchezaji gani amefunga magoli mengi zaidi kuanzia mwezi Agosti hadi Septemba.
Kwa maelezo zaidi unaweza kupitia katika ukurasa wetu wa Tunzo.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x