Sambaza kwa marafiki....

Moja ya dhumuni kuu la tovuti yetu ni kusheherekea mafanikio ya watu ambao wanafanya vizuri katika ulimwengu huu wa soka kwa Tanzania. Hivyo basi zifuatazo ni Tunzo ambazo tovuti hutoa kwa Wachezaji, Makocha na Wadau wa mpira wa miguu. Unaweza kubofya kwenye maelezo zaidi ili kujua jinsi utaratibu ulivyokuwapata washindi na orodha ya waliowahi kushinda.

Galacha wa Mabao wa Kandanda kwa Mwezi

Tunzo hii yenye lengo la kusheherekea mafanikio ya ufungwaji mabao, huangalia tu ni mchezaji gani ambaye amefunga idadi kubwa kupita wenngine ndani ya mwezi mmoja katika Ligi Kuu ya Tanzania bara kwa wanaume pekee.Hutolewa mara moja tu kwa mwezi.

Ikiwa wachezaji wamefungamana magoli, mchezaji aliyecheza mechi chache ndio atakuwa galacha wa magoli. Pia ikiwa wamefungamana kwa idadi ya mechi, itaangaliwa mchezaji gani amechea dakika chache zaidi.

Galacha wa Mabao wa Kandanda kwa Msimu.

Tunzo hii huangalia rekodi ya nani Mfungaji wa Mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa Ligi Kuu ya Mpira wa miguu Tanzania bara kwa Wanaume tu.

Ikiwa wachezaji wamefungamana magoli, mchezaji aliyecheza mechi chache ndio atakuwa galacha wa magoli. Pia ikiwa wamefungamana kwa idadi ya mechi, itaangaliwa mchezaji gani amechea dakika chache zaidi.

Mpikaji Mabao Bora

Tunzo hii huangalia nani anaongoza kwa kusaidia kutoa pasi za mwisho zilizozaa bao. Na zitatolewa kwa mwezi na kwa msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania bara kwa wanaume.(Kwa sasa hazijaanza kutolewa)

Galacha wa Kandanda

Tunzo hizi ni mahususi kwa wachezaji, wadau na makocha wa mpira wa Miguu wanaocheza Tanzania (Ligi yoyote) na Wachezaji Watanzania walio nje ya Tanzania wakicheza soka la kulipwa. Rasmi itaanza 2020, lakini imekuwa na majaribio kidogo mwaka 2019 kwa waliofanya vizuri 2018. Tunzo hii inaangalia mafanikio na ‘perfomance’ kwa mwaka mzima (Januari hadi Disemba) tu.

Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz