Sambaza....


Klabu ya Manchester United inakaribia kumsajili kiungo mshambuliaji raia wa Brazil, Anderson Talisca katika majira haya ya joto, jarida la Sportwitness la Uturuki limeripoti.

Kiungo huyo wa Benfica ya Ureno yupo nchini Uturuki kwa mkopo katika katika klabu ya kandanda ya Besitkas Kwa misimu miwili sasa.

Taarifa zinasema Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amekuwa akimuhusudu kiungo kwa muda mrefu sasa na kutokana na kiwango bora alichoonesha msimu huu kwa kufunga mabao 20 kunamfanya Kocha huyo ashindwe kuvumilia na kuahidi kumnyakua kipindi hiki cha kiangazi.

Mashabiki wa Man Utd wameshaanza pia kumfuatilia Talisca

Kuna Makubaliano yoyote? 

Mpaka sasa Manchester United hawajakubaliana lolote na Benfica kuhusu usajili wa Talisca, wakati ambapo mkataba wake unamruhusu kusajiliwa mazima na Besiktas jambo ambalo litakuwa rahisi kwa Manchester United kumsajili.

Hata hivyo tetesi zinasema Manchester United wameandaa ofa ya Euro 40M (Tsh 10 Bilioni) kwa ajili ya kumnasa Talisca ambaye naye ameonesha nia ya kufanya kazi na Jose Mourinho.

Sambaza....