Sambaza....

Jana timu ya soka ya Alliance Schools kutoka Mwanza ilikuwa inacheza na timu ya Simba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Simba iliifunga Alliance Schools magoli 5 kwa 1.

Katika mchezo huo ambao ulianza kuwa na hali ya kutofautiana kati ya kocha mkuu wa Alliance Schools na Mmiliki wa timu hiyo ya Alliance Schools ambaye pia ni manager wa Timu hiyo, James Bwire.

Wawili hawa walitofautiana baada ya Mkurugenzi huyu ambaye pia ni manager , Bwana James Bwire kuoneshwa kutoridhika na kikosi cha kwanza kilichopangwa na Mbwana Makata katika mchezo huo.

Hivo aliamua kukipangua kikosi hicho na kuweka wachezaji ambao aliona wanafaa kuwepo katika kikosi cha kwanza kwa ajili ya kupambana na Simba.

Kitu ambacho kilisababisha kocha mkuu wa Alliance Schools kukasirika na inadaiwa ameiacha timu hiyo na kurudi nyumbani kwake.

Kandanda.Co.Tz italifuatilia suala hili mpaka mwisho wake.

Sambaza....