Ligi Kuu

Molinga akipungua kilo 4 ‘ataua watu’- Zahera

Sambaza....

Baada ya Jana David Molinga kufungua akaunti yake ya magoli kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba FC ya jijini Mwanza, kocha mkuu wa Yanga , Mwinyi Zahera amedai kuwa sasa mshambuliaji huyo atakuja kuwa wa moto.

Akizungumza na kituo cha Azam TV baada ya mchezo huo, kocha huyo alidai kuwa alichokuwa anakikosa David Molinga ni hali ya kujiamini tu.

“Leo kafunga goli moja na amekosa magoli mawili lakini baada ya muda atazidi kujiamini zaidi. Akipewa mechi nyingi atazidi kujiamini zaidi na atakuwa na uwezo mkubwa zaidi. Mimi ndiye niliyemsajili naamini uwezo wake”.

Alipoulizwa kuhusu kupungua uzito kwa David Molinga. Mwinyi Zahera alidai kuwa kwa sasa amepungua kilo na amebakiza kilo nne tu.

“Awali alikuwa na kilo 78 kwa hiyo amebakiza kilo nne apungue ili akae vizuri. Hapo ndipo utakapoona uwezo wake mkubwa atakaouonesha “-alidai kocha huyo kutoka Congo.

Yanga inajiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco ya Zambia utakaochezwa tarehe 14/09/2019 katika uwanja wa Taifa


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.