Blog

Mshambuliaji wa Stars asajiliwa Uingereza!

Sambaza....

Nyota ya mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Addi Yusuph amepata dili jipya na kuingia kandarasi na timu nyingine nchini Uingereza.

Addi Yusuph aliejumuishwa katika kikosi cha Mwalimu Amunike kwaajili ya michuano ya Afcon ameikacha timu yake ya Saohil na kusaini kwa klabu yake mpya Blackpool fc.

Add Yusuph akiwa katika uwanja wa nyumbani wa klabu yake mpya

Add Yusuph amesaini mkataba wa miaka miwili huku kukiwa na uchaguzi wa kuongeza mwaka mmoja zaidi pia. Kwa kusajiliwa na Blackpool anakua mchezaji wakwanza kusainiwa na klabu hiyo kwa msimu huu wa usajili.

Blackpool inayoshiriki League One nchini Uingereza imemaliza nafasi ya kumi msimu huu wa Ligi huku wakiwa na alama 62. Ligi hiyo inashirikisha baadhi ya vigogo wa zamani wa EPL kama Sundarland na Portmouth.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.