
Nyota wa zamani wa klabu ya Ndanda fc Atupele Green amefanikiwa kufunga mabao matatu yaani Hatrick katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya klabu yake ya Biashara United dhidi ya KMC.
Atupele amefunga mabao hayo jana na kuiwezesha klabu yake kushinda mabao manne kwa sifuri mbele ya KMC katika uwanja wa Karume Musoma na kujihakikishia alama tatu kwa Wanajeshi hao wa mpakani.

Atupele Green mchezaji wa zamani wa Yanga sc na Ndanda kwa kufunga mabao hayo anakua mchezaji wa sita msimu huu kuweza kufunga mabao matatu katika mechi moja.
Wachezaji wengine walifunga hatrick msimu huu ni pamoja na Meddie Kagere (Simba sc), Obrey Chirwa (Azam fc), David Ulomi (Alliance School), Daruesh Saliboko (Lipuli fc) na Kevin Kongwe Sabato (Kagera Sugar).
Unaweza soma hizi pia..
Alli Kamwe: Lengo Yanga na sio Mayele!
Mayele ni mchezaji muhimu kwenye Timu. Yanga inamuhitaji zaidi akiwa Fiti uwanjani kuliko yeye anavyokihitaji kiatu cha Ufungaji bora kabatini kwake.
Msemaji Simba: Mambo ni magumu!
Kila mwanasimba anatakiwa kufahamu hilo na kukubali mambo ni magumu.
Kola na mfupa uliomshinda Mayele!
Licha ya Fiston Mayele kusifiwa na kuoneoana ni moja ya washambuliaji hatari katika Ligi lakini hakufanikiwa kufunga
George Mpole anaishi ndoto zetu!
juhudi binafsi za George Mpole na ndio maana utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa ni 1 kwao lakini yeye pekeake Mpole ana mabao 13.