Yikpe
Uhamisho

Mshambuliaji Yanga: Niliwaambia wasimsajili Yikpe.

Sambaza....

Mshambuliaji nyota wa zamani wa Yanga raia wa Kenya Boniface Ambani  ameweka wazi ni jinsi gani alikataa Yanga isimsajili mshambuliaji raia wa Ivory Coast Yikpe kutoka Gor Mahia ya Kenya.

Ambani aliyeichezea Yanga kwa misimu miwili na kufunga zaidi ya mabao 40 amefunguka jinsi alivyokuwa akiwasihi viongozi wa Klabu yake ya zamani ya Yanga kutomsaini mshambuliaji huyo, ambaye amefanikiwa kufunga bao moja tu tangu afike klabuni hapo.

Mshambuliaji wa Yanga Yikpe akipambana na mlinzi wa Kagera Sugar Juma Said Nyosso

Boniface Ambani “Ndio niliwaambia wasimsajili, nikawaonya wasimsaini mshambuliaji (Yikpe) na sasa kila mtu analia. Wao [haswa mashabiki] wanataka kujua ni nani aliyesababisha [Yikpe] kutia saini na nilikuwa nimewaonya juu ya kusaini kwake.”

“Nilimwangalia akiwa Gor Mahia. Mimi ni mshambuliaji na ninajua sifa ya washambuliaji ambao Yanga wanapenda. Nilijua hatastahili kufiti pale. Nimemwangalia mara kadhaa, kukimbia kwake ni hafifu, kugusa kwake kwanza ni hafifu, siku zote huwa anakosa malengo na umaliziaji wake sio mzuri ” Alimalizia Boniface Ambani.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.