AFCON

Msuva: Nafasi ya kufuzu Afcon ipo wazi.

Sambaza....

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Simon Msuva amesema wamejiandaa vyema wao kama wachezaji na wapo tayari kupambania matokeo dhidi ya Uganda.

Msuva amesema wanakwenda kukutana na mchezo mgumu lakini kwa uwepo wa mashabiki pamoja na wao wachezaji basi watapata matokeo mazuri dhidi ya Uganda.

Simon Msuva “Tuna mchezo mgumu kesho ila mchezo wa kwanza tumeshaumaliza na tumepata matokeo mazuri lakini kiuhalisia bado hatujamaliza. Katika mchezo wa kesho tunawahitaji sana mashabiki tunawaomba Watanzania mje kwa wingi kiwanjani ili muweze kutupa sapoti.”

Simon Msuva mfungaji wa bao pekee dhidi ya Uganda katika mchezo wa ugenini.

Nyota huyo wa zamani wa Wydad Casablanca na Yanga amesema wao kama wachezaji wanahimizana kuelekea mchezo huo kwani bado nafasi yakufuzu ipo wazi kwa timu zote.

“Kikubwa kesho tunatakiwa tupambane ili tuweze kukaa vizuri kwenye kundi letu maana timu zote bado zina nafasi ya kusonga mbele na kufuzu,” alisema Simon Msuva

Kuelekea mchezo huo kati ya Tanzania na Uganda tayari TFF wametangaza jukwaa lote la mzunguko mashabiki wataingia bure kabisa na hii ni kutokana na juhudi kubwa za wadau mbalimbali wa soka na serikali kununua tiketi kwa mashabiki ili wakaiunge mkono timu yao ya Taifa.

 


Sambaza....