Blog

Mtakatifu Luca Modric hana baya.

Sambaza....

Mwamba leo amecheza mechi yake ya mwisho ya Kombe la Dunia na kuiongoza Croatia kumaliza nafasi ya tatu kwenye fainali hizo lakini heshima aliyoiweka ni zaidi ya msemo ‘HANA BAYA.’

Akiwa na miaka sita baada ya baba yake kufariki vitani (Bosnia War) alionekana moja ya watoto wanaopenda soka lakini hakuaminiwa na baadhi ya akademi alizoenda kufanya majaribio kutokana na umbo lake dogo na kutokuwa mwenye nguvu.

Luca Modric (kulia) akiitumika Croetia katika mchezo wa mshindi wa tatu dhidi ya Morroco katika michuano ya Kombe la Dunia.

Kama ipo ipo tu, Modric aliendelea kucheza kwenye maeneo ya ukimbizini alipokuwa akiishi kimasikini na mama yake baada ya mshua wake aliyekuwa fundi makenika wa jeshi la Croatia kwenye vita ya Bosnia kuuawa na kubaki bila makazi.

Katika ndondo zake za mtaani aliendelea kukusanya kijiji, kufunga na kupiga pasi za usahihi na kuwaaminisha watu kuwa umbo lake dogo sio shida kwenye soka na baadae akaonwa na mabosi wa Dinamo Zagreb na kumsaini kwenye akademi yao.

Luca Modric akiwa na uzi wa Dynamo Zagreb.

Akiwa Dinamo alizidi kufanya kazi nyepesi kwake(soka) na baadae akatolewa kwa mkopo Zrinjski Mostar kisha Inter zapresic kabla ya kurudi Dinamo mwaka 2015 na kuanza kubonda timu ya wakubwa.

Alicheza kwa mafanikio makubwa Dinamo ikiwamo kutwaa makombe matatu mfululizo ya ligi na kuwa MVP wa ligi hiyo mwaka 2017 na baada ya hapo alitua England ndani ya Tottenham Hotspurs na kilichofuata hapo ni Dunia kuimba ‘LUCK LUKA’ jina lake la utani.

Kiungo wa Real Madrid Luca Modric.

Mwaka 2012 alijiunga na Real Madrid anayoichezea hadi sasa na akiwa pale amezidi kuionyesha Dunia kuwa soka ni kazi rahisi kwake, uongozi ni kipaji kwake, miguu yake ‘ina macho’ na nguvu sio chochote kwenye soka.

Achana na makombe kibao aliyobeba, Moja ya kumbukumbu nzuri zaidi kwa Modric ni kuvunja ubabe wa Ronaldo na Messi wa miaka isiyopungua 10 kwa kuwatupilia mbali na kutwaa tuzo ya Ballon d’Or.

Luca Modric

Anaachana na Kombe la Dunia akiwa bado na ufundi wake, amelicheza kwa misimu minne tofauti, mechi 20, fainali moja. HANA BAYA KIUNGO.

HUNA BAYAA LUCA LUKA⚽️✊🏾.

Sambaza....