Ligi Kuu

Mtibwa , Mwadui na Ruvu Shooting wafungiwa !

Sambaza kwa marafiki....

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imezifungia vilabu vya Mtibwa Sugar, Mwadui Complex na Ruvu Shooting kutumia viwanja vyao kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara.

Akizungumza na mtandao huu wa Kandanda.co.tz, mtendaji mkuu wa bodi ya ligi kuu Tanzania bara, Boniface Wambura amedai kuwa viwanja hivo vimefungiwa kutokana na Club Lincensing.

“Tumevifungia viwanja hivo kwa sababu ya Club Lincensing, ukiangalia Club Lincensing inataka viwanja viwe vimezungushiwa matofali”.


Tunakundalia: Vilabu gani vinatakiwa kucheza Ligi Kuu Tanzania?


“Lakini vilabu hivi viwanja vyao havijazungushiwa matofali, uwanja wa Manungu na uwanja wa Mabatini vimezungushiwa na mabati, wakati uwanja wa Mwadui Complex umezungushiwa senyenge”- alidai mtendaji huyo bodi ya ligi kuu.

Uwanja wa Manungu

Uwanja wa Mwadui Complex

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.