Ligi Kuu

Mtibwa waibwekea Singida United.

Sambaza....

Kikosi cha timu ya soka ya Mtibwa Sugar (wanaTamTam) chini ya kocha wake Zubeir Katwila kimeendelea na mazoezi  katika uwanja wake wa nyumbani wa Manungu Complex, Turiani kujiandaa na mchezo ujao wa ligi kuu bara (TPL) dhidi ya Singida United mchezo utakaochezwa Jumanne hii mkoani Morogoro.

Kuelekea mchezo huo afisa habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru Ligalambwike amesema kikosi cha Mtibwa Sugar kimejiandaa vilivyo kuhakikisha wanaendelea kuwapa furaha wakazi wa Morogoro na viunga vyake lakini kubwa zaidi wapenzi wa Mtibwa Sugar popote Tanzania.

“Tumejiandaa kwa ajili ya kuwapa raha tu wana Mtibwa hakuna namna nyingine, timu sasa hivi ina uwezo mkubwa na morali yake iko juu sana hivyo kila anayekuja katikati ya mashamba haya ya miwa ajiandae na kipigo maana vijana wanatandaza soka la hali juu sana” amesemaKifaru

Singida United walipanda ligi kuu msimu 2017/2018 na walikutana na Mtibwa Sugar mara tatu katika msimu huo na Mtibwa walifanikiwa kushinda michezo miwili na sare 1 michezo miwili ilikuwa ya ligi kuu na mmoja fainali ya kombe la shirikisho.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.