Raphael Obafemi wa Mwadui fc akipambana na Bakari Mwamunyeto wa Coastal Union.
Uhamisho

Mwamunyeto anaweza akafanya vibaya Yanga

Sambaza....

Dau la milioni 250 limemtoa Bakari Nyundo Mwamunyeto kutoka Coastal Union kwenda Yanga. Dau ambalo ni kubwa , ukubwa wa dau hili unakuja kwa mchezaji ambaye ni mzawa.

Ilikuwa ni ngumu sana kwa kipindi cha nyuma kuona mchezaji mzawa akisajiliwa kwa kiasi kikubwa cha pesa. Kwa dau hili linamfanya Bakari Nyundo Mwamunyeto kuwa mchezaji ghali mzawa kuwahi kutokea kwenye ligi yetu.

Pia Bakari Nyundo Mwamunyeto anaenda kuwa beki ghali kuwahi kutokea kwenye ligi yetu. Kitu hiki ni kizuri sana kwenye soka letu. Hii ni ishara soka letu linaelekea uelekeo wa kuwa biashara inayolipa.

Biashara hii inaweza ikawa nzuri sana kwa Bakari Nyundo Mwamunyeto nje ya uwanja kwa sababu amepata pesa ambazo zinaweza kumsaidia kwa kiasi kikubwa kwenye maisha yake.

Swali kubwa ambalo anatakiwa kulijibu ni namna gani ambavyo anaweza kuonesha kiwango kikubwa kinachotokana na pesa ambazo amepewa kama za usajili.

Presha kubwa inabaki kuwa kwake. Mashabiki wa Yanga watataka kuona akicheza kulingana na kiwango cha pesa ambacho amesajiliwa .

Kwa hiyo anaenda Yanga huku akiwa na presha ya deni la hii pesa iliyotumika kumsajilia. Asipokuwa makini kuna uwezekano mkubwa wa yeye kutocheza katika kiwango kikubwa


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.