Uhamisho

Namungo yaanika vifaa vipya!

Sambaza....

Klabu ya soka ya Namungo fc yenye maskani yake Ruhangwa mkoani Lindi wamelitumia vizuri dirisha dogo baada ya kuwaongeza baadhi ya wachezaji ili kuzidi kujiimarisha katika Kombe la FA na Ligi Kuu Bara.

“The Southern Killers” wamesajili jumla ya wachezaji  watano wapya huku pia wakiwaacha wachezaji watano na kuwatoa kwa mkopo wachezaji watatu.

Nyota wapya waliosajiliwa na Namungo fc ni pamoja na Jamal Mwambeleko (KCB- Kenya),  Edward Charsel Manyama (JKT Tanzania), Rodgers Gabriel ( Mwadui fc),  Mwisho Yangson (Boma Fc) na Frank Zakaria kutoka Singida United.

Jamal Mwambeleko amejiunga na Namungo Fc!

Pia nyota watano walioachwa na klabu hiyo ni pamoja na  Toure Sie Leopard, Sina Jerome, Omary Mponda, Abduwaeeh Adesola na Juma Ally Babjey.

Huku pia ikiwatoa kwa mkopo wachezaji watatu Selemani Bwenzi (Greenwories),  Paul Ngalema (Lipuli fc) na Steven Mganga kwenda Mbeya city.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.