Ligi Kuu

NBC imetimiza wito wetu

Sambaza....

Ni takribani miaka mitano sasa toka mtandao huu uone umuhimu wa kuwa na bima kwa wachezaji wa Ligi Kuu. Imechukua muda mrefu lakini ni mafanikio makubwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

》》Ujumbe kwa mameneja Masoko

Benki ya NBC imezindua Huduma ya Bima ya Maisha na Afya kwa Wanamichezo.

Benki ya NBC ambayo ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya NBC imezindua huduma mpya ya Bima kwa wanamichezo mahususi kwa wachezaji, benchi la ufundi pamoja na familia zao wakilenga kuwahakikishia huduma bora za kiafya wachezaji wanaoshiriki Ligi kuu ya NBC hususani pindi wanapota majanga ya kiafya.

Huduma hii inapewa amana na Kampuni za Bima ya Britam na Sanlam inahusisha Bima ya Afya na Maisha vile vile itahusisha wachezaji 640 wanaoshiriki Ligi kuu ya NBC, benchi la ufundi pamoja na familia zao.

Mchezaji akitolewa baada ya Kuumia

Ikumbukwe kuwa baadhi ya wachezaji wameshindwa kuendelea na mpira wa miguu baada ya kuumia au pia baadhi kuona hakuna maana ya kuucheza mpira huu pendwa. NBC, kwa bima hii inatengeneza mazingira mazuri kwa familia ya mpira. Kwa haraka wachezaji 640, inamaana kuna wahusika zaidi ya 2,560 wanaenda kunufaika katika mpango huu.

“Tukio hili tumelipokea vizuri sana, baadhi ya wachezaji wanaumia tena maumivu makubwa wanashindwa kupata huduma ya tiba kutokana na ukosefu wa fedha za kuwahudumia” Alisema Masau Bwire – Afisa Habari | Ruvu Shooting

Ligi kuu sasa inaelekea kuwa tamu zaidi, iwafungue wadau wengine kwaajili ya kuifanya ligi yetu bora.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.