ASFC

Ni Lipuli na Azam fc kwenda Ilulu

Sambaza....

Michuano ya Azam Sports Federation Cup inaelekea tamati baada ya nusu fainali ya pili kupigwa leo na kumpata mshindi atakaekwenda kucheza fainali katika uwanja wa Uhuru mkoani Lindi.

Baada ya Azam fc kutangulia fainali katika nusu fainali ya kwanza dhidi ya KMC kwa ushindi wa bao moja kwa sifuri sasa ni zamu ya Wanapaluhengo.

Lipuli fc imefanikiwa kuifunga Yanga sc na kukata tiketi ya kwenda fainali kumenyana na Azam fc mkoani Lindi  katika dimba la Ilulu baada ya kuifunga mabao mawili kwa sifuri.

Magoli ya Lipuli yamewekwa kimiani na Paul Nonga “Baba mchungaji” na Miraji Athumani “Shevishenko” katika dakika A 33 na 40 kipindi cha kwanza cha mchezo.

Ikumbukwe mshindi wa michuano hii ya Azam Sports Federation Cup anapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Shirikisho barani Africa.

Msimu uliopita ilikua ni fainali kati ya Singida utd na Mtibwa Sugar ambapo Mtibwa ndio waliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa mawili katika dimba la Sheikh Amri Abeid Arusha!

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.