EPL

Ni mapema kwa Manchester United kukitupa kinanda cha Sanchez

Sambaza....

Kuna mwanadamu mmoja aliwahi kukaa chini akafikiria sana kisha akaja na msemo mmoja ambao mpaka leo unatumika kwenye kizazi hiki. “More Expectations hurt”, yani matarajio makubwa huumiza. Unaweza kufikiria kipi kilichomsukuma mpaka akaja na huu msemo ? Alifanywa nini?, ni kipi ambacho alitarajia lakini kwa bahati mbaya hakikutokea kwenye maisha yake mpaka akakaa chini akaja na huo msemo ?

Msemo ambao mpaka leo unaishi kwenye maisha yetu kama wanadamu. Hapana shaka sisi wanadamu tumekuwa tukiishi kwenye huu mstari. Mstari wa kutegemea makubwa sana kwenye vitu ambavyo tunavisubiri na mwisho wa siku kunapotokea kitu ambacho ni kinyume na matarajio yetu maumivu husogea karibu na mioyo yetu. Mioyo yetu hufubaa, mioyo yetu husinyaa kwa kujikunyata kwa huzuni. Na wakati mwingine majuto na machozi huwa ni kitu cha kawaida tu.

Na hii ni kwa sababu wanadamu tumezaliwa na matumaini. Hupenda kutumaini sana vitu vizuri vitokee kwenye maisha yetu, na huu ndiyo huwa mwanzo wa sisi kuumia.

Sanchez

Mwanzo ambao ulifanyika katika jiji la Manchester United. Jiji ambalo lina timu ambayo ina mashabiki wengi duniani. Hii ni timu pendwa duniani.

Hakuna ubishi kwenye hili, inapendwa sana na inafuatiliwa sana kwa sababu tu ina mashabiki wengi dunuani.

Mashabiki ambao walizoea kuishi kwenye pepo. Pepo ambalo lilitengenezwa na Sir. Alex Ferguson. Kocha ambaye aliacha alama kubwa katika maisha ya Manchester United.

Alama ambazo zimebaki katika mioyo ya mashabiki wa Manchester United, ndiyo maana mashabiki wengi wa Manchester United wanaamini vitu vizuri wameumbiwa wao.

Makombe wameumbiwa wao, wachezaji bora wameumbiwa wao. Ndiyo maana ilikuwa sherehe kubwa sana kwa ujio wa Sanchez pale Manchester United.

Dunia ilisimama. Mchezaji mkubwa na mwenye kipaji kikubwa alikuwa anakuja katika jiji la Manchester United. Hawakusita hata kumpa jezi namba 7.

Jezi ambayo ni nembo katika klabu ya Manchester United kwa sababu tu imewahi kuvaliwa na magwiji waliowahi kufanya vizuri pale Manchester United.

Matumaini yao makubwa yalikuwa kumuona Sanchez akifanya vizuri ndani ya jezi hiyo lakini kwa bahati mbaya hakufanya vizuri.

Wengi wanaonekana kumchoka na hawataki kabisa kuendelea naye. Umeiangalia michuano ya Copa America?

Sanchez hajaisha , na ni mapema sana kumchoka. Anatakiwa apewe mwaka mwingine wa kuaminiwa ili adhihirishe kuwa hajachoka.Ni mapema kwa Manchester United kukitupa kinanda cha Sanchez

Kuna mwanadamu mmoja aliwahi kukaa chini akafikiria sana kisha akaja na msemo mmoja ambao mpaka leo unatumika kwenye kizazi hiki.

“More Expectations hurt”, yani matarajio makubwa huumiza. Unaweza kufikiria kipi kilichomsukuma mpaka akaja na huu msemo ?

Alifanywa nini?, ni kipi ambacho alitarajia lakini kwa bahati mbaya hakikutokea kwenye maisha yake mpaka akakaa chini akaja na huo msemo ?

Msemo ambao mpaka leo unaishi kwenye maisha yetu kama wanadamu. Hapana shaka sisi wanadamu tumekuwa tukiishi kwenye huu mstari.

Mstari wa kutegemea makubwa sana kwenye vitu ambavyo tunavisubiri na mwisho wa siku kunapotokea kitu ambacho ni kinyume na matarajio yetu maumivu husogea karibu na mioyo yetu.

Mioyo yetu hufubaa, mioyo yetu husinyaa kwa kujikunyata kwa huzuni. Na wakati mwingine majuto na machozi huwa ni kitu cha kawaida tu.

Na hii ni kwa sababu wanadamu tumezaliwa na matumaini. Hupenda kutumaini sana vitu vizuri vitokee kwenye maisha yetu, na huu ndiyo huwa mwanzo wa sisi kuumia.

Mwanzo ambao ulifanyika katika jiji la Manchester United. Jiji ambalo lina timu ambayo ina mashabiki wengi duniani. Hii ni timu pendwa duniani.

Takwimu za Sanchez akiwa na Arsenal FC

Hakuna ubishi kwenye hili, inapendwa sana na inafuatiliwa sana kwa sababu tu ina mashabiki wengi dunuani.

Mashabiki ambao walizoea kuishi kwenye pepo. Pepo ambalo lilitengenezwa na Sir. Alex Ferguson. Kocha ambaye aliacha alama kubwa katika maisha ya Manchester United.

Alama ambazo zimebaki katika mioyo ya mashabiki wa Manchester United, ndiyo maana mashabiki wengi wa Manchester United wanaamini vitu vizuri wameumbiwa wao.

Makombe wameumbiwa wao, wachezaji bora wameumbiwa wao. Ndiyo maana ilikuwa sherehe kubwa sana kwa ujio wa Sanchez pale Manchester United.

Dunia ilisimama. Mchezaji mkubwa na mwenye kipaji kikubwa alikuwa anakuja katika jiji la Manchester United. Hawakusita hata kumpa jezi namba 7.

Jezi ambayo ni nembo katika klabu ya Manchester United kwa sababu tu imewahi kuvaliwa na magwiji waliowahi kufanya vizuri pale Manchester United.

Matumaini yao makubwa yalikuwa kumuona Sanchez akifanya vizuri ndani ya jezi hiyo lakini kwa bahati mbaya hakufanya vizuri.

Wengi wanaonekana kumchoka na hawataki kabisa kuendelea naye. Umeiangalia michuano ya Copa America?

Sanchez hajaisha , na ni mapema sana kumchoka. Anatakiwa apewe mwaka mwingine wa kuaminiwa ili adhihirishe kuwa hajachoka.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x